0

Mhe Mgana Msinda akiwasalimia wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA

Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai jana alijiunga na Chadema na kutambulishwa katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema.

Mgana, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Iramba Mashariki (2000-2010) alitambulishwa pamoja na Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Goodluck Ole Medeye na ofisa mwandamizi wa chama hicho, Matson Chizii.

Makada hao wa CCM jana usiku waliambatana katika kikao hicho na aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowassa.

Habari zinasema kuna makada zaidi wa CCM watakaotambulishwa katika mkutano mkuu wa Chadema leo.

Post a Comment Blogger

 
Top