By Fidelis Butahe (Mwananchi)
Njombe. Mgombea urais wa Chadema kwa mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano atatumia fedha itakayopatikana katika uzalishaji wa gesi kama sehemu ya kutekeleza ahadi ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu ambayo ipo katika ilani ya uchaguzi ya Ukawa, huku akisisitza, “Msiogope.”
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kituo cha polisi cha mji wa Makambako mkoani hapa, Lowassa alisema mbali na gesi atatumia fedha zitakazopatika katika zao la pamba huku akihoji zilivyotumika fedha ambazo serikali ya awamu ya nne imekopa katika nchi wahisani.
Kivutio kingine katika mkutano huo alikuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye ambaye alitumia mtindo wa kuwauliza wananchi, “CCM” na wao kujibu “Ni shiiiida”, kueleza mambo matatu yaliyofanywa na serikali ya CCM na kusababisha watanzania waishi kwa matabaka.
“Tumetengeza ilani kiboko ambayo ndani ya miaka mitano Tanzania yetu itabadilika, lazima tupunguze tabaka kati ya tajiri na masikini kwa uchumi wa pamba, chai, dhahabu na gesi kwanini tushindwe. Mkitupa ridhaa na Mungu akikubali tukakwenda kasi na tutakuwa na maendeleo.
Lowassa alisema akiwa rais kuanzia Januari mwakani wanafunzi hawatalipa chochote na elimu itakuwa bora, atahakikisha walimu wanalipwa madai yao yote, sambamba na watumishi wengine wa serikali.
Akizungumza katika mkutano huo Sumaye alisema Watanzania wamepata shida mpaka kufikia wakati wanaamini shida ni sehemu ya maisha yao, huku akisema nchi ya Libya iliingia katika matatizo kwasababu utawala uliokuwepo ulikataa kuwapisha wengine kuongoza nchi na kukandamiza watu.
Soma zaidi habari hii kesho kupitia Mwananchi E-Paper
Post a Comment Blogger Facebook