Eddy  alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia  darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka  kumwambia kitu muhimu....
Endelea...
Doreen  alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili  sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy..  Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi  kuziteka hisia za Eddy haswa. 
Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
  
Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
"Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.
"Naam"
"niambie basi.."
"ah!..  Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka  uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya  chini ili majirani wasiweze kusikia.
"Eddy!  we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen  alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata  Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa  Dorice.
"Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "
"Na Dorice je?"
"habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"
"mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.
"Nikubalie  Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi  yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen  alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.
"Okey! nakubali kuwa na wewe!"
"Oh  my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu  mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani  walikuwa darasani.
"Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."
"sharti gani tena?" Eddy alishtuka
"upo tayari?"
"ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"
"good.. nafurahi sana"
"Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.
"usijali nitakuambia baadae..."
Alisema  Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha  sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara  aliachia tabasamu.
Ilikuwa  ni mchana majira ya SAA nane na nusu ambapo kengele iligongwa katika  shule ya sekondari Mabango ambapo iliwaataarifu wanafunzi wote kuwa muda  wa vipindi umekwisha na ni muda wa kupata chakula cha mchana.
Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.
Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.
"Mkuu  wa shule mama Dayana Mbeshi ameaga dunia Leo asubuhi kwa kifo cha  ghafla kilichompata ofisini kwake..pia walimu wawili wana hali mbaya na  wamefikishwa hospitalini kwa matibabu!" ilikuwa sauti ya masikitiko sana  kutoka kwa Mwalimu Gallus iliyoonesha simanzi nzito sana aliyokuwa  nayo.
Mwalimu  huyo alishusha pumzi ndefu sana na kuendelea " Maombi yenu in muhimu  sana kwa walimu wenu ambao wapo hospitali... na..." mwalimu Gallus alishindwa kuendelea kuzungumza kwani machozi yalikosa adabu yakashuka kwa kasi hivyo akaamua kuondoka eneo lile.
Wanafunzi  wote waliondoka lakini mwishoni alibaki Eddy alitembea taratibu huku  picha ya msichana katili anayejifanya mwema, Doreen ikizidi kumjia  akilini mwake na kumfanya aisahau kabisa njaa aliokuwa nayo. Njia nzima  alkuwa akizungumza peke yake kama mwehu mpaka alipofika bwenini.
  
"Ah  Doreen! ni msichana mzuri sana! siamini kama amekuwa wangu..!" Aliwaza  Eddy huku akiachia tabasamu kisha akabadili nguo na kujitupa kitandani. 
Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.
Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.
*******
Dorice  alikuwa amekaa kitandani kwake huku machozi yakitiririka mashavuni  mwake. Weupe wa ngozi ya USO wake ulibadilika na kuwa mwekundu kutokana  na kulia kwa muda mrefu, hakuamini kama Eddy angemtenda kiasi kiasi  kwani siku zote aliamini Eddy ndiye MTU pekee wa kumuamini, aliamini  kama Eddy ndio furaha pekee ya moyo wake iweje Leo amtupe kama taka ya  msafiri ndani  ya basi pale airushapo kupitia dirisha bila kujua  itakapotua? Alimuona Eddy kama mnyama katili asiyekuwa na moyo wa utu.
Marafiki zake Dorice walizidi kumbembeleza atulie bila mafanikio yoyote.
"Kwa alichonifanyia Doreen, siwezi kumwacha kilahisi tu... lazima nimfanyie kitu..." Alijiapiza Dorice
  
"  Ni lazima atajuta mpaka kifo chake... hatokaa anisahau kwa  ntakachomfanyia.. lazima aelewe kuwa Mimi ni Dorice mtoto wa Kinyaturu  sinyang'anywi tonge mdomoni kwa urahisi!" Alizidi kujiapiza Dorice akiwa  amejifunika blanket mpaka usoni. Lakini baada ya muda mfupi Dorice  aliinuka kitandani pale na kujifuta machozi kisha akapiga hatua za  haraka kuelekea nje.
********
Mke wa Mwalimu John amuijia  Juu Mumewe akitaka kujua suruali ile imetoka wapi. Lakini mwalimu John  hakutaka kuweka wazi kile kilichomkumba shuleni.. alitaka iwe siri yake  mpaka atakapofanikiwa kwenda Malawi kutafuta waganga wakumroga  aliyemfanyia uchuro.
  
"John! umefumaniwa huko sio?" alifoka mke wa John
"usipaniki  mke wangu tulia.. sijafumaniwa mim!" alijitetea mwalimu John bila  mafanikio na wakati huo tayari mkewe alishaanza kumtandika makofi mumewe  na alipoona haitoshi akanyanyua upawa na kumtandika nao Mwalimu John  kichwani.
  
Ghafla John akanyong'onyea na kutulia kimya kitini bila kutikisika..
"John! John!" aliita mke wa mwlm John bila mafanikio John hakuweza kuitikia.
"Mime wangu... John wangu" alizidi kuita lakinu John alikuwa kimya, mkewe alichanganyikiwa sana.............

 
Post a Comment Blogger Facebook