0


Kijana mwenye mkia wa sentimita 20 uliyoota chini ya uti wa mgongo wake amefanyiwa upasuaji ili kuondoa mkia huo ambao Ulianza kujitokea katika mgongo wa kijana huyo mwenye miaka 18 baada ya siku yake ya 14 kuzaliwa.

Yeye na familia yake kutoka Nagpur nchini India walifanya swala hilo kua siri kwa sababu walikuwa na wasiwasi angechokozwa na wenzake, na sasa wanataka kuonana na daktari baada ya mkia huo kuendelea kukua na kuota mfupa kwa ndani.

Mkia huo unadaiwa kuwa mrefu kuwahi kutokea kwa mwanadamu licha ya kuwa kesi kama hivyo ni vichache.

Madaktari wanasema kuwa kijana huyo huenda aliota mkia huo ndani ya tumbo la mamake kutokana na kasoro katika uti wa mgongo, lakini ukaja kuonekana nje baada ya kijana huyo kuwa mkubwa.

Post a Comment Blogger

 
Top