1


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.

“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania”

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini kuchukua hatua katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao ili visitoweke.

Makamu wa Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya nchi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda alisema mkutano huo wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Post a Comment Blogger

  1. How to Play Real Money Slots - Oklahoma Casinos
    Real money 토토 사이트 중계 slots online 유니벳 are usually 스보벳 offered 토토 라이브 스코어 at casinos online. You can find a variety of game categories from traditional casino slots and video 슬롯 머신 게임 poker to

    ReplyDelete

 
Top