0
Vanessa Mdee aliwekwa kwenye Kikaango cha EATV wiki hii ambapo mashabiki wake walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wake na Jux na mipango yao ya baadaye.

Akijibu swali la mipango aliyonayo na Jux, muimbaji huyo alisema wanatarajia furaha ya kudumu huku akidai kuwa hawana mpango wa kuwa na mtoto siku za hivi karibuni.

Pia Vanessa alidai kuwa amekuwa na uhusiano na Jux kwa mwaka mmoja na miezi minne sasa.

Kuhusu collabo ba Diamond, Vee Money alisema itakuwepo muda si mrefu na anaamini kuwa itakuwa ya kuotea mbali.

Kuna mtu alimuuliza kama ana beef yoyote na Alikiba na Vanessa kujibu, “Ali Kiba sina beef naye infact sina beef na mtu yeyote. Nampenda nakumheshimu sana. Hatujawahi kufanya kazi ya mziki pamoja lakini ninamuamini sana ana kipaji sanaa na cha kipekee. Tunashirikiana kupinga ujangili kama mabalozi wa Wild Aid.”

Kuhusu kama bado anaendelea kufanya kazi na MTV Base, Vanessa alijibu, “Mdee Nimeacha kufanya vipindi vya kawaida nafanya vipindi maalum tu kama interview ya Neyo nilioifanya katika tuzo za MAMA 2015.”

Post a Comment Blogger

 
Top