0
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu atoke mahabusu, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda amemuomba Rais John Magufuli kutimiza ahadi yake ya kushughulikia hali ya kisiasa visiwani Zanzibar. Ponda amemtaka Rais Magufuli kutekeleza ahadi yake aliyoitoa bungeni juu ya kufuatilia hatma ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na kutoa tamko la yale yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kutafuta suluhu yaliyokuwa yakihusisha pande mbili zinazovutana za Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).“Rais achukue ahadi yake aliyoitoa bungeni, ana wajibu wa kuitekeleza kwa vitendo na ahakikishe mzozo huu anaupatia ufunbuzi bila ya kuitumbukiza Zanzibar kwenye dhiki na uhasama,” alisema Ponda. Pia alisema vyombo vya usalama vilivyopo Zanzibar vipo kwa amri yake hivyo endapo patatokea jambo lolote kabla ya kumaliza mzozo wa kisiasa uliopo visiwani humo ni yeye atakayelaumiwa.

Post a Comment Blogger

 
Top