0


Kiungo wa Manchester United, Mjerumani Bastian Schweinsteiger, ambaye ameonekana kukosa nafasi kwa kocha Jose Mourinho, amesema hafikirii kujiunga na timu nyingine ya barani Ulaya, na badala yake ataenda kucheza soka katika Ligi ya Marekani au Asia.
Bastian Schweinsteiger (5)
Schweinsteiger alitumia account yake ya instagram kutoa taarifa kwamba Manchester United ndio itakuwa klabu yake ya mwisho kuitumikia barani ulaya, akisisitiza United ndio klabu pekee ambayo ingeweza kumuondoa Allianz Arena. Hivyo kwa sasa ataendelea kubaki Manchester na kocha atakapomhitaji basi ataenda kuitumikia klabu.

Post a Comment Blogger

 
Top