0
Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka ‘High Tible Sound’ Barnaba Classics amewataka wasanii wenzake kuwekeza nguvu nyingi kwenye kuandaa audio za nyimbo zao.
barnaba
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Barnaba amesema wasanii wanajikuta wanaweka nguvu kubwa kwenye kuandaa video kubwa kuliko audio hali ambayo amedai inashusha muziki wa Tanzania.
“Asikudanye mtu muziki mzuri unapatikana kwenye audio nzuri,” alisema Barnaba. “Ukifanikiwa kuandaa audio kali sasa ndo ufikirie issue ya video,lakini unakuta wasanii sasa hivi wanatumia nguvu kubwa kuandaa video kuliko audio, mimi nataka kuwaambia kitu kikubwa kwenye muziki ni audio, mengine baadae,”
Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo ‘Lover Boy’ hivi karibuni amewataka wasanii kuwekeza nguvu nyingi kwenye audio kuliko kwenye video.

Post a Comment Blogger

 
Top