
Msafara  wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu  Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo  ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao  wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.
Ajali  imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya  wilaya ya Mtwara .Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi  wanne wa Makamu wa Rais.
Awali  kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia  na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel  ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

 
Post a Comment Blogger Facebook