Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya tatu ( kama hukuisoma bofya hapa)
 Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
 Sehemu ya nne 
.... DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.
"hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?" Dorice aliropoka kwa hasira.
"  nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng'ang'ania  mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione  nimekukaushia!" Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno  ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga  machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake  kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka  kulitia DOA penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.
"Ama  kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu  kipenzi Leo unageuka adui yangu!"alisema Dorice huku akipiga hatua na  kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati  na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.
"we vipi? hebu niache niondoke?"
"nitakuachaje  sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?" alisema Doreen kwa  kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni  mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.
"umefanikiwa  kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu.... haya Fanya  lolote utakalo tena ili kunyang'anya haki yangu ya mapenzi... do it!"  alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana  na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen  yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.
"hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy... sijui unanielewa?"
Dorice  hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua  kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa  mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana. 
Alijibadilisha  macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni  alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen  alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali  alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana  bila yeye mwenyewe kujitambua.
"hebu  niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya"  alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia  kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.
Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.
**********
Walimu  wote walikuwa hawaelewi mambo yanayoendelea shuleni pale, kwani kila  siku liliibuka jipya. Suala la mwalimu John kuvuliwa suruali kwa  mazingira ya kutatanisha lilizidi kuwapa maswali mengi walimu wa while  ya sekondari mabango mpaka wakaogopa hata kuingia madarasani, kwani  walihisi wanaweza kudhalilishwa kama ilivyomtokea mwalimu John.
Mbali na suala hilo pia suala la mkuu wa shule kujifungia ofisini liliwapa mtihani mkubwa kwani haikuwa kawaida yake.
"jamani  nimeenda ofisi ya mkuu wa shule karibia Mara tatu nimegonga sana lakini  hakutoa jibu hata nilipojaribu kusukuma mlango inaonekana amefunga kwa  ndani!" alisema makamu mkuu wa shule baada ya kuingia staff.
"hata  Mimi nimeenda pale ofisini lakini palikuwa kimya sana ingawa mlango  unaonekana umefunguliwa kwa nje... nimepiga simu haipokelewi" alisema  mtaaluma.
kiukweli iliibuka sintofahamu miongoni mwa walimu wote waliingiwa na hofu kubwa.
" mmh! hii sio kawaida ya mkuu kabisa inabidi tufanye jambo"
"Mimi naona tuvunje mlango tu" alipendekeza mwalimu wa nidhamu.
walimu  wote walikubaliana kuvunja mlango wa ofisi ya mkuu wa shule. wakaebda  moja kwa moja mpaka ofisini kwa mkuu na kuvunja mlango kisha wakaingia..  walichokutana nacho kila MTU hakuamini , walibaki midomo wazi huku  machozi yakiwadondoka kama chemichemi katikati ya mlima.
Mwili  wa mwalimu Mbeshi ulikuwa umeoza vibaya sana funza walitapakaa kila  mahali wakisindikizwa na harufu mbaya iliyojaa ofisini mle. hakuwa  mbeshi tena mwanamama aliyejipenda na kunukia marashi muda wote Bali  jina lilibadilika na kuwa maiti.
Walimu  walitulia kimya kwa muda wa dakika mbili nzima Vila kusema chochote  lakini macho ya makamu mkuu wa shule yalitua mpaka mezani kwa mbeshi  ambapo aliona karatasi ndogo nyeupe yenye ujumbe. Akaisogelea na  kuichukua, kisha akaanza kuisoma. Ghafla alishtuka sana baada ya kusoma  ujumbe ule "UNAFATA WEWE ULIYESOMA KARATASI HII."
Makamu  yule kwa woga na hamaki akaropoka " Mimi sijasoma chochote...  tusisingiziane hapa!" alisema huku akificha macho yake na kumkabidhi  mtaaluma karatasi ile kwani walimu wote hawakujua kilichotokea hivyo  wakatamani wasome ujumbe uliokuwemo mle.
********
Dorice alimtuma MTU amwitie Eddy darasani lakini mwanafunzi yule akakataa. hivyo Doreen aliamua kwenda mwenyewe darasani mle.
Darasa  lilikuwa limetulia kimya sana, Dorice akafungua mlango na kuingia  lakini ghafla alipoingia wanafunzi wote darasani mle wakacheka kicheko  kikali sana kilichomtia hofu sana Dorice. lakini akajikaza kisabuni  licha ya kwamba alijua wanamcheka yeye, akamsogelea Eddy na kumtaka  watoke nje lakini Dorice aligundua mabadiliko makubwa sana kwa Eddy Ila  hakuuliza chochote wakatoka nje. wanafunzi wakacheka tena kwa dharau  kitendo kilichomuumiza sana Dorice.
"hivi we demu unajisoma??" alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
"Eddy! sijakuelewa!"
" unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?" maneno ya Eddy yalimfanya Dorice ataharuki.....

 
Post a Comment Blogger Facebook