0

 Wezake wote wakahamaki kila mmoja hakuamini kuona tukio lililopo mbele yao,Rahab akatupa shoka chini na kuwatazama wezake usoni kwa umakini
“Munacho ogopa nyinyi ni nini?”
“Ehee ahaaa hapana” Halima alijibu kwa kubabaika
“Tuutoeni sasa huu mwili”
“Tutaupeleka wapi?”
“Mimi ninaona tukodishe taksi”
“Dereva gani ambaye atakubali kubebea maiti?”
“Sasa itakuwaje?”
Wote wakakaa kimya wakitafakari ni nini cha kufanya,Fetty akawatazama wezake kwa umakini kisha akazungumza kwa sauti ya kujiamini
“Nisikilizeni....Cha msingi ni kumkata kata kama nyama ya bucha kisha tunamuweka kwenye kisafleti na kwenda kumtupa tunapo pajua sisi”
“Mmmmm”
“Agnes usigune unadhani kuna mtu anataka kwenda jela wakati kama huu....mimi bado ninayapenda miasha ya uraiani japo yanachangamoto kama hizi”
“Basi  tuanzeni kuifanya hiyo kazi”
Wakavua nguo zao na kila mmoja akabakiwa na chupi na sidiria na kila mmoja akachukua kitu ambacho anaamini akikata kwenye mwili wa binadamu kitakata,Wakambeba Mama Bonge hadi bafu lililomo ndani ya nyumba na kuanza kumkata kata kiungo kimoja bila huruma
“Angekuwa ngombe huyu mama nahisi saa hizi si chini milioni tungekuwa tumesha pata”
“Anna hembu acha uchizi wako”
“Kweli nawaambia...Huyu mama angekuwa ni ng’ombe ahaa mbona tungepata mshiko wa maana”
“Alafu si ninasikia kuna makabila wanakula nyama za watu?”
“Mmmmm kabila gani hizo?”
“Wapo ila nahisi Tanzania hakuna”
“Tanzania mbona wapo?”
“Kabila gani?”
“Wachawi”
Agnes akaachia msunyo baada ya Fetty kuzungumza pointi isiyo na msingi wowote,Wakaendelea kumkata kata mama Bonge huku wakipiga story za aina mbalimbali hadi wakamaliza kumchangua changua,wakachukua safleti pamoja na vifuko vya nailoni na kuweka viuongo kadhaa kwenye kila kifuko na kuvifunga na vyote kwa pamoja wakavidumbukiza kwenye safleti.
Wakaanza kufanya usafi kila sehemu yenye damu na wakamaliza.Wakaoga kwa pamoja na kuvaa nguo nyingine zilizo watoa tofauti na laiti ukikutana nao barabarani huwezi kujua kama niwauaji
“Jamni safari ya wapi?”
“Kuna mzungu mmoja juzi kati nililala naye yupo maeneo ya mbezi bichi twendeni kwake”
Rahab alizungumza na wote wakakubaliana,wakakodi taksi huku safleti yao wakiingia nayo ndani ya taksi na dereva hakuelewa chochote kinacho endelea.Wakamlipa ujira wake dereva na Rahab akampigia simu dokta William ambaye yupo Tanzania kwa kazi maalumu ya utoaji wa mafunzo ya oparesheni za sura kwa madkatari wa jeshi tu,Dokta Wiliam akaminya kitufe kinacho liruhusu geti la mlangoni kwake kufunguka na Rahab akawa kiongozi wa masafara na wote wakaingia ndani.
“Mmmm Jamani hapa kama ulaya geti linajifungua lenyewe”
“Anna acha ushamba unataka kusema kutembea kuto huko hujaona geti kama hili?”
“Sijawahi”
“Ahee shosti nawe umezidi ushamba”
“Tuachene na hilo je hii safleti niiweke wapi kwa maana nimechoka kuibeba”
“Idumbukize hapo kwenye hayo maua”
Halima akaidumbukiza safleti kwenye maua yaliyo tengenezwa vizuri kisha wakaingia kwenye jumba la dokta Wiliam.
“Ohhh karibuni warembo”
Dokta William alizungumza kwa Kiswahili cha kujing’ata nga’ta na Rahab akamkumbatia Dokta William na kumpiga mabusu ya kinafki kisha wakajibwaga kwenye masofa ya dhamani yaliyomo mule ndani
“Rahab ona wewe leo fanyia mimi Suprize”
“Ndio mpenzi wangu nimekuja kukufanyia Suprize na wezangu ili kama tukikukuta na msichana tumpige sana”
“Mimi wezi saliti wewe kutokana moyo wangu penda sana wewe,shindwa hata fanya kazi kwa mambo yako ya kukatika kitandani fanya mimi Crayz”
Wote wakacheka huku wakimtazama Dokta William
“Usijali kama ni kiuno tuu utakipata leo hadi uimbe wimbo wa Taifa la nchi yako”
“Kweli?”
“Ndio kwani kuna siku ambayo nimeshawahi kukudanganya?”
“Ahhaa utafanya mimi nisirudi nyumbani maana nyinyi Afrika munajoto sana tofauti na wanawake ngozi nyeupe wao baridi sana kama amfibia(viumbe wenye asili ya kuishi kwenye maji)”
“Tuachane kwanza na hilo.....sisi tumekuja kuhamia kabisa hapa kwako na kama unavyo tuona na vibegi vyetu hatuna sehemu sisi ya kwenda wala ya kulala”
“Kuna mashaka jumba lote hili kaa mimi peke yangu tena ona raha kuona sichana rembo kama nyinyi kuja kaa na mimi nitapata burudani kedekede”
“Ni wewe tu ila ninaombi jingine?”
“Ombi gani?”
“Tunaomba gari yako hiyo ya UN twende nayo sehemu mara moja kisha tunarudi?”
“Mbali sana na hapa?”
“Hapana sio mbali kivile na hapa”
“Basi ngoja niwapeleke turudi tufanye sherehee kubwaa”
Rahab akawatazama wezake na wakakubaliana kwa ishara na wote kwa pamoja wakasimama na kuacha vitu vyao,Agens akaichukua safleti yenye mwili wa mama Bonge na wakaingia kwenye gari aina ya pick up Ford na wakamuomba dokta William waelekee nje ya jiji kidogo.
“Sasa hivi saba usiku huko kwenda fanya nini?”
“Kuna mzigo tunakwenda kuutupa”
“Nini tena?”
“Ni mwi......”
“Rahab”
Fety alimzuia Rahabu hakumalizia anacho taka kukizungumza kwa maana kinaweza kikaleta mtafaruku baina yao na mzungu huyu.
“Zigo gani hiyo?”
Dokta William aliuliza huku akiongeza kasi ya gari hadi na kuliacha jiji la Dar es Salaam,
“Ahaa ni mzigo wa kawaida tuu mpenzi wangu wala usijali katika hilo”
“Isije ikawa dawa kulevya”
“Ahaa mpenzi wangu umeona wapi mtu akatupa dawa za kulevya wakati ni dili kabisa hilo”
“Mbona wezako kaa kimya hawapigi story”
“Ahaa wemejichokea kwa maana mama mwenye nyumba wetu leo ametutimua ndio hivyo hatuna pa kwenda”
“Ahaa sasa mimi huku Pwani kuna handaki langu kubwa kama hamtojali nyinyi kaa humo kwa siku kama mbili tatu kisha rudi mjini kwa maana pale nyumbani kwangu kesho fika wakuu wangu toka state of America sasa shindwa nyinyi juiwapi kaa”
“Ehee tena itakuwa vizuri”
“Eti warembo nyinyi mpo tayari kukaa kwenye handaki?”
“Ni wewe tu”
Ndani ya nusu saa gari yao ikaingia kwenye msitu mnene na kutokana na uwezo wa gari haikuweza kukwama kwenye matope yaliyo sababishwa na mvua iliyokuwa ikinyesha asubuhi.Wakasimama kwenye moja ya mti na Dokta William akashuka ndani ya gari na kutembea hatua chake na kufungua mfuniko mmoja wa chuma ambao juu yake kulikuwa  na majani mengi ambayo sio rahisi kwa mtu kuuona mfuniko huo,Akawaita Rahab na wezake na wote wakashuka kwenda chini kwa kutumia ngazi zilizopo kwenye eneo hilo.
Dokta William akawasha taa zenye mwanga mweupe unao kufanya uone kama ni mchana kweupe,Akawasha mashine inayo sambaza hewa ya oksijeni kwenye eneo zima la handaki,Katika handaki lake kuna vyumba nane ambavyo vinne ni vyakulala na vitatu vimehifadhia vifaa vingi ikiwemo bunduki za kivita.
Kila huduma inayo hitajika kwenye nyumba kwenye hili handaki ipo na zimetengenezwa vizuri na kutakufanya ukiishi ndani humo usiwazie kama upo ndani ya pango,Dokta William akawaelekeza jinsi ya matumizi ya badhi  ya vitu ikiwemo jinsi ya kuzitazama kamera za ulinzi zilizo fungwa mbali na eneo la kuingilia hapa msituni kwa kupitia computer zilizomo humu ndani.Dokta William akaondoka alfajiri na mapema kurudi zake Dar es Salaam na ikawa ni nafasi nzuri ya Rahab na wezake kuvizika viungo vya mama Bonge 
                                           *****
Maisha yakazidi kwenda mbele huku kila siku jioni Dokta William akija kuwatembelea Rahab na wezake na kuwafundisha baadhi ya mbinu za kijeshi kwani Dokta William na miongoni mwa wanajeshi wanaotegemewa sana katika jeshi la umoja wa mataifa UN.Kadri siku zinavyo zidi kwenda ndivyo jinsi Rahab,Agnes,Anna,Halima na Fety walivyo zidi kukomaa katika mafunzo ya kijeshi ambayo Dokta William aliamua kuwafundisha ili kuwatumia katika biashara zake haramu anazo zifanya akishirikiana na baadhi ya viongozi serikalini.
“Amini sasa nyinyi kuwa wanajeshi kamili si ndio?”
“Ndio”
“Sasa hapa kuna kazi moja taka nyinyi anza kuifanya kwa umakini na umahiri wa hali ya juu...”
Dokta William alizungumza huku akiwa amesimama kwenye kitambaa cheupe kikubwa huku mwanga mkali unaotoka kwenye kifaa kidogo(projectar) na kuna picha mbili za wanaume zikiwa zinaonekana kwenye kitambaa hicho.
“Hapa kuna watu wawili.....Huyu mmoja anaitwa Karim Yussuf  ni mmiliki wa Sheli za Total kwa hapa Tanzania.....na huyu namba mbili yeye itwa Mansuri ni mfanya biashara wa madini mkoani Arusha na kabla ya kesho kutwa mimi sitaki waona hawa watu kwenye dunia hii”
“Dokta kwahiyo unataka sisi tuwaue hao?”
“Ndio nataka ua huyo Karim sasa hivi yeye yupo Dar kwenye hoteli Serena na huyu Mansuri yeye yupo Tanga hoteli moja itwa Tanga bich resolt”
“Cha kufanya ni nyinyi kwenda kukamilisha hii kazi ndani ya masaa 20 yajayo hawa watu wawe wamefutika kwenye ramani ya dunia”
“Samahani Dokta je hawa watu wana makosa gani hadi sisi tuwaue hilo ni swali namba moja,swali namba mbili je utatuhakikishia vipi usalama wetu na tatu malipo yatakuwaje?”
“Swali zuri Anna...Malipo kila mmoja wenu nitampa milioni kumi shillings na kwakitangulizi nitawapa milioni tano tano kila mmoja,Mbili usalama wenu upo sababu hiyo kazi si yangu ila imetoka ngazi za juu na tatu hata mimi nilipo uliuliza ni kosa gani walilo fanya hawa watu nikaambiwa nikafanye kazi hiyo”
Halima akashusha pumzi nyingi huku akiwatazama wezake ambao wameridhika na kazi hiyo ya mauaji.
“Hakikisheni munafwata kanuni zote za nilizo wafundisha katika mauaji ya kimya kimya kama mutashindwa basi tumieni silaha zozote na hakikisheni mikono yenu munaivalisha gloves ili kuepuka kuacha alama za vidole kwa hao maiti”
“Je na sura zetu tuzaziwekaje?”
“Agnes hapo mutajua ni jinsi gani ya kucheza huo mchezo wa sura zenu na hizi ndizo namba zao za simu”
Dokta William akawatajia namba za simu za watu wanaopaswa kuuawa ndani ya masaa 20.Rahab na Agnes wakapangiwa kwenda Tanga kwenda kumuua Mansuri.Halima,Anna na Fety wakapangiwa kwenda Dar es Salaam kumuua Karimu.Dokta William akawakabidhi gari Rahab aina ya Verosa yenye rangi nyeusi kisha Walio baki akaongozana nao hadi Dar es Salaam huku wote wakiwa amekamilika katika swala zima la silaha.
                                         ******
Kwa mwendo wa masaa manne kutoka mkoa wa Pwani hadi Tanga ukawafanikisha Rahab na Agnes kufika Tanga na moja kwa moja wakaelekea kweneye Hotel ya Tanga beach Resolt na wakachukua chumba kimoja na kuanza kumtafuta Muntar ni wapi alipo.Wakiwa wamejipumzisha pembezoni mwa swimming pool lililopo kwenye hoteli hii wakamuona Muntar akiingia hotelini akiwa ameongozana na wapambe wake wapatao sita wanao mlinda na wanaonekana wapo makini sana kwa kila mtu ambaye anapita karibu na bosi wao.
“Ag mtu mwenyewe ndio yule pale”
“Nimemsoma wangu so tunalianzisha sasa hivi?”
“Hapana tutumie akili nyingi kumuua la sivyo hatuto toka salama humu ndani”
“Una wazo gani kichwani?”
“Uzuri wetu unaweza pia ukampagawisha?”
“Je ni mtu wakupenda wanawake isije tukajipendekeza ikala kwetu”
“Ngoja tuyasome mawazo yake”
Agnes na Rahab wakaanza kumfwatilia Muntar na watu wake kwa kutumia macho ya wizi ambayo wanahakikisha hakuna anaye weza kugundua juu ya swala hilo.Muntar na watu wake wakatafuta sehemu iliyo tulia na kukaa na kuagiza vinywaji.Agnes akasimama na kuishusha suruali yake ya jinzi chini kidogo na kuziachia shanga zake za kiunoni kuonekana vizuri na kwamwendo wa madaha akajipitisha pembeni ya meza ya Muntar na watu wake na kuwafanya watu wa Muntar wabaki wakimkodolea macho ya uchu Ages.
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzia vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi wake analo lihitaji...
 ITAENDELEA....

Post a Comment Blogger

 
Top