0
Chege Chigunda ameamua kuweka kambi ya mwezi mmoja nchini Afrika Kusini kwaajili ya maandalizi ya collabo yake na wasanii wawili wa kimataifa.

Akizungumza na Bongo5 akiwa nchini humo, Chege amesema mmoja wa wasanii atakaowashirikisha anatoka Nigeria na mwingine kutoka Afrika Kusini.

“Mimi nipo huku South Africa hii nafikiri ni wiki ya pili na nitaendelea kuwepo huku kwa wiki moja na nusu,” amesema. “Kwahiyo nitakaa huku kama mwezi hivi na kitu kilichonileta huku ni kwaajili ya kufanya recording ya ngoma yangu mpya ambayo nimeamua kuwashirikisha wasanii wawili tofauti kutoka nchi mbili tofauti Nigeria na South Africa na nitawataja baadae ni wasanii gani,” ameongeza.

“Lakini nimefanya collabo ambayo imeshirikisha nchi tatu, Tanzania, South Africa na Nigeria, na plan ni kwamba sihitaji kurudi mpaka ifanyike video na mipango ipo safi na management yangu inalishughulikia hilo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.”

“Kwahiyo hatua tuliyofikia tumesharekodi mimi nimeshaingiza vocal zangu na MSouth Afrika ameshaingiza tayari. Nigeria nafikiri wiki hii ndo wataweka vocal from Nigeria halafu baada ya kuweka ngoma watafanya mixing then tutaanza kufanya mipango ya video kwa sababu kuna ile MTV Awards wasanii wa Nigeria watakuja kwaajili hiyo. Kwahiyo nitatumia opportunity hiyo kufanya video,” amesisitiza muimbaji huyo.

Katika hatua nyingine Chege amedai kusikitishwa na taarifa kuwa amefariki ambazo amedai zinaweza kusababisha matatizo kwa ndugu zake.

“Watu wanaandika taarifa ambazo sio nzuri na sio za kweli ambazo zinadisappoint watu, zinadisappoint mashabiki. Kuna mtandano nasikia unaitwa ukweli mtupu, nasikia wameniandika mimi nimefariki, wakati mimi mzima, naendelea na kazi zangu hawajui hata nipo wapi, wanakurupuka wanaweka picha za kwenye movie. Silalamiki sana kwa sababu hivyo ni vitu vinavyopangwa na mwenyezi Mungu na naamini wanavyoandika upuuzi wananiongezea maisha marefu. Lakini pia naona ni stupid kwa sababu wanaandika vitu ambavyo ni nonsense. Huwezi kuwa umesoma na umefungua blog yako halafu unaandika vitu ambavyo havina akili. Ni kitu ambacho sijapenda na nimewadharau sana.”

“Hawa wameikosea jamii, unaweza ukamfunga mtu, hizo picha ni za toka miaka minne iliyopita na movie ya Nonini, unakurupukaje kuandika mtu amekufa? Mtu anashindwa kujua na mimi nina wazazi! Wanaweza wakawa na presha mtu unaandika fulani kafa, mama yake akiona au kusikia itakuwaje? Mimi niko mbali uku unavyoandika hivyo mama yangu anaweza akafikiria vipi? Au familia yangu inaona ghafla, South Africa kuna story mbaya, unaandika na kuweka picha ambayo inaonyesha damu, wewe unaweka fulani amekufa, wazazi wakiona itakuwaje? Wazazi wetu watu wazima unajua.”

Source bongo5

Post a Comment Blogger

 
Top