0
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia ( Young Shepolopolo) inawasili Tanzania Alhamisi kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya wenyeji Tanzania (Tanzanite) kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kugombea kufuzu kucheza kombe la Dunia la wanawake chini ya miaka 20 litakalofanyika mwakani nchini Guinea Bissau.
Timu hizo zitashuka dimbani siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kikosi cha timu ya Tanzanite chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kimeweka kambi eneo la Mbande na kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Azam Complex kwa takribani wiki ya pili sasa kujiandaa na mchezo huo.
Msemaji wa Shirikisho la soka nchinin Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema hali ya kambi ya Tanzanite ni nzuri wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ya ya hali ya juu, kikubwa Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Msejai wa kuwapa sapoti timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 watakapokuwa wakicheza na wenzao wa Zambia.
 She-polopolo wanatarajiwa kuwasili jioni kwa usafiri wa ndege wa shirika la Rwanda ambapo Ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.
 Mchezo huo utachezwa siku ya jumamosi majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi, ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Dunia za Wanawake chini ya miaka 20 (U-20) zitakzofanyika nchini Papua New Guninea mwaka 2016.
Mwamuzi wa mchezo huo ni Batol Mahjob kutoka nchini Sudan, akisaidiwa na washika kibendera Remaz Osaman na Walaa Bilal, mwamuzi wa akiba Khadmallah Elasayed wote kutoka nchini Sudan na Kamisaa wa mchezo ni Flora Roosevelt kutoka nchini Malawi.

Post a Comment Blogger

 
Top