0
Mfalme wa Bongo Crunk, Cpwaa amesema kuwa mwezi ujao anategemea kuachia wimbo mpya ambao utakua na ladha ya Bongo Fleva ambayo anadai wasanii wengi wameitelekeza kutokana na kuiga muziki wa Nigeria.

Cpwaa bado anafanya muziki, Cpwaa bado ni king wa bongo crunk,na safari hii nikija nakuja kuwapa kile kitu watu ambacho wamekimiss.” Cpwaa ameiambia Bongo5.

“Mimi mwenyewe nafatilia muziki kila siku naangalia video za watu nasikiliza radio naangalia Tv naangalia blog, yaani watu wanafanya vitu vile watu wanaigana tu, bado Unigeria too much, majina ya nyimbo hata hayajulikani yanamaanisha kitu gani, kwahiyo kuna umuhimu wa kurudisha ile original Bongo Fleva.”

Cpwaa ameongeza kuwa wimbo ambao ataachia mwezi ujao amemshirikisha msanii wa Bongo ambaye hakupenda kumtaja kwa sasa.

“Mwezi wa nane naachia wimbo mpya baada ya ukimya wa muda mrefu, wimbo ambao nitakuwa nimemshirikisha msanii wa hapa hapa nyumbani siwezi kumtaja jina kwa sasa lakini muda ukifika nitawajulisha wapenzi wangu kwamba ninatoa wimbo na nani. Najua watu hawajanisikia siku nyingi wanajiuliza maswali mengi…muda wote huu nilikua kimya nimerekodi nina nyimbo zangu ambazo ziko tayari.”

Katika hatua nyingine Cpwaa amesema kuwa album yake ya pili iko katika hatua za mwisho kukamilika.

“Vile vile album yangu ya pili almost imekamilika, kwahiyo nina nyimbo za kutosha za kuachia sasa hivi mpaka mwakani, nilichokuwa nafanya natengeneza misumari natulia huku nashughulika na mambo mengine ambayo yamekuwa yakinikeep busy ambayo hayahusiani na muziki…so watu wasiwe na wasiwasi.”

Ameongeza kuwa pia amefanya collabo na baadhi ya wasanii wa nje.

“Muendelezo wa kufanya nyimbo za kimataifa uko pale pale, kuna collabo ambazo nimefanya na wasanii wa nje sitaki kutaja majina saizi.”
Chanzo B5

Post a Comment Blogger

 
Top