0
majambazi wanne walifariki dunia jana tunduma wilayani momba baada ya kurushiana risasi na askari kwa mda wa masaa nane. kati ya hao majambazi mtanzania mmoja na wazambia watatu

Tukio hilo lilitokea maeneo ya chapwa ambapo majambazi wanne ambao walikua wanamiliki siraha kali walipata ajali baada yakumvamia mfanyabiashara mmoja sogea anaefahamika kwa jina la Tadeo.
huyu ni jambazi ambae aliwasumbua mapolisi kuliko majambazi wote akiwa kwenye gari la peke yake

majambazi hao walimteka na kumfungia stoo na kumnyang'anya silaha yake na kiasi cha pesa na kukimbia.
majambazi hao walichukua gari la Tajiri huyo na kutokomea nalo lakini wananchi waliwaona na kuanza kuwatilia mashaka.

Majambazi hao walikimbia umbali wa kilomita mbili na kupata ajali pale walipotaka kukata kona na kuelekea porini wakidhani wanafukuziwa na gari inayofahamika kama kenta ingawa haikuwa hivyo
Mjambazi hao waliamua kukimbia kwa mguu ingawa mmoja wao aliumia mguu na kushindwa kukimbia vizuri. wanachi waliendelea kuwakimbiza ingawa majambazi walipiga risasi mbili hewani ili kuwatawanyisha.
Askari wa jeshi la polisi walifika baada ya dakika kumi na kusaidiana na wananchi waliokuwa wakiwakimbiza. baada ya kukimbilia milimani ndipo walipoanza kurushiana risasi na polisi na kuweza kkuwauwa majambazi wote.
Raia wawili ambao waliongozana na askari walipata majeraha mmoja akiwa ameppigwa risasi ya mguu huku mwingine akipigwa jiwe kichwani.
viongozi wa jeshi la polisi wamewapongeza wananchi kwa kazi walioifanya maana bila wao wasingefanikisha tuikio hilo. majambazai hao wal;ik,utwa na ticketi ya basi iliyoonyesha waliwasili masaa machache kabla ya kufanya uhalifu huo. silaa na pesa alizonyang'anywa tajiri huyo hazijapatikana ingawa zile zilizotumika na majambazi zilipatikanavideo ya majambazi hao
https://youtu.be/fkzdU-egtYU mkuu wa wilaya akizungumza na wananchi juu ya tukio hilo

Post a Comment Blogger

 
Top