Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye,  leo  amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Umoja wa Katiba  ya Wananchi (UKAWA).
Sumaye amejiunga rasmi na Ukawa wakati  wa mkutano wa wanahabari na viongozi wa Umoja huo,  mkutano uliofanyika  mchana wa leo katika ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar.
Aidha Sumaye hakusema ni chama gani  amejiunga nacho, licha ya kubainisha lengo lake kuu la kuondoka CCM ni  kwenda kuimarisha Ukawa na kuongeza nguvu kwenye vyama vya upinzani hasa  katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
 
Post a Comment Blogger Facebook