0
Kijana Fred Bryson Mmari anayedaiwa kufanywa ndondocha na familia yake.
KILIMANJARO: Kha! Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Naomi Bryson anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Wilaya a Sia, Kilimanjaro huku mumewe, Bryson Mmari (56), akisakwa kwa madai ya kumfungia ndani na kumfanya ndondocha mtoto wao wa kwanza, Fred Bryson Mmari (31) kwa zaidi ya miaka mitatu.

Tukio hilo la aina yake, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye Kijiji cha Karanzi wilayani Sia Mkoa wa Kilimanjaro.

SIMULIZI INAANZA
Jumatatu hiyo, mtoa taarifa mmoja alipiga simu Global Publishers na kusimulia kisa cha ajabu ndani ya nyumba aliyokutwa Fred.Alisema kwa muda mrefu amekuwa akiona watu wanane walioficha sura zao wakiingia kwenye chumba alichofungiwa kijana huyo na kuongea lugha isiyojulikana.
 Mtoto huyo akipanda gari la polisi
“Iliniwia vigumu kujua nini kinachoendelea katika chumba hicho, lakini siku moja, usiku nikiwa nimetoka nje kujisaidia, niliwaona watu hao, mmoja alimulika tochi ndani ya chumba. Ndipo nilipomwona mtu mwenye nywele nyingi, nikabaini kuwa, ndani ya chumba hicho kuna mtu anaishi kwa siri,” kilisema chanzo.

MAMA MWENYE NYUMBA AULIZWA
“Siku moja niliamua kumuuliza mama mwenye nyumba ambapo aliniambia kuwa ni mtoto wake mkubwa Fred. Ndipo na mimi nilipoamua kutoa taarifa kwa jamii na kwenu.”

AMANI, POLISI ENEO LA TUKIO
Baada ya kujulishwa madai hayo mazito, gazeti hili liliambatana na askari nane kutoka Kituo cha Polisi Sia mpaka nyumbani kwa mwanamke huyo.

MWENYE NYUMBA AHAMAKI
Bada ya polisi kuvamia, mama mwenye nyumba alihamaki pale alipoamrishwa kufungua chumba hicho kilichokuwa kimefungwa kwa kufuli.

MTU WA AJABU AONEKANA
Awali, mwanamke huyo huku akiwa na wasiwasi aligoma kufungua akisema hana funguo na kwamba ni chumba ambacho yeye haruhusiwi kufungua lakini askari hao wenye silaha walimwamuru ndipo alipotii. Baada ya kufungua, kijana huyo alitoka kwa kasi hadi nje.

ASKARI WADHIBITI
Askari walifanikiwa kumdhibiti kijana huyo ambaye alikuwa haongei kwa ufasaha. Walimrudisha ndani ya chumba chake.
Mama akiingia kwenye gari la polisi.
HALI NDANI YA CHUMBA
Mazingira ya chumba hicho yalisikitisha kama kweli aliishi binadamu kwa miaka mitatu kwani kulikuwa na kinyesi, mkojo na damu. Mwanamke huyo alijifunika uso kwa aibu.

MAMA ASIMULIA KWA POLISI
Alipobanwa, mwanamke huyo alisema alilazimika kumfungia ndani ya chumba hicho mtoto huyo baada ya kuwa na ugonjwa wa akili ambao aliupata miaka mitatu iliyopita wilayani Rombo mkoani hapa akiwa anafanya kazi saluni.

SWALI GUMU
Alipoulizwa ni kwa nini hawakumpeleka hospitali kwa kipindi chote cha miaka mitatu na kumwacha kwenye chumba kichafu huku akila kinyesi, mwanamke huyo alijibu kwa mkato: “Nilijisahau.”

BABA AZUNGUMZA YA KUSHANGAZA
Akizungumza kwa simu, mzee Mmari alikana kumfanya ndondocha mtoto wake ila ana matatizo ya akili na walilazimika kumweka kwenye chumba hicho chenye harufu mbaya kwa vile harufu hiyo humfanya aache usumbufu.

JIRANI NAYE ANENA
Naye jirani mmoja (jina lipo) alisema walipokuwa wakiulizia alipo Bryson, walijibiwa kwamba, alishafariki dunia hivyo wao kubaki na mshangao.

TAMKO LA POLISI
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sia, Joseph Bashigwa alisema wanamshikilia mwanamke huyo, pia wanamsaka mzee Mmari ambaye alikimbia muda mfupi baada ya askari kufika. Kuhusu Fred, alisema wamempeleka hospitali ya wilaya kwa uchunguzi wa afya.

Post a Comment Blogger

 
Top