0
Staa wa filamu Riyama Ally anatarajia kufunga ndoa na msanii chipukizi wa muziki ‘Mysterio’ ambaye amekaa nae katika uchamba kwa muda mrefu.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Ijumaa hii, Riyama alisema tayari mwanaume huyo ameshamtolea posa.

“Mimi na my wangu tupo kwenye mahusiano ya uchumba lakini mungu akipenda Insha’Allah tutafunga ndoa, kwa sababu ndoa zinapangwa mbinguni.” alisema Riyama.

Hata hivyo, Riyama hakuweka wazi tarehe rasmi ya kufunga ndoa.

Aidha, Riyama amezungumzia kubadili mtindo wake wa uigizaji, kupita filamu yake mpya ambayo ipo njiani kutoka, ikiwa tayari imepatiwa jina ‘Mke Gani’.

Post a Comment Blogger

 
Top