Akizungumza na Ripota wetu katika eneo la tukio mtaa wa Sakina mkuu wa operesheni wa TFDA Benson Mcheza anasema wamefanikisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kwamba mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria na kulipia gharama zote za kuteketeza bidhaa hizo
Kwa upande wake mfanyabiashara anayemiliki kiwanda hicho Chalo Makala amesema bidhaa zilizoko kwenye ghala ni bidhaa za dukani kwake ambazo amelipia kodi zote stahiki na kwamba zile anazozalisha zilikua kwenye majaribio.
Kwa upande wa uongozi wa kata ya Kiranyi kilipo kiwanda hicho wakatoa wito kwa jamii kutoa taarifa mapema pale wanapobaini uendeshaji wa biashara yoyote kinyume cha sheria ili kuepusha madhara kwa watumiaji lakini pia kuziba mianya ya ukwepaji kodi.
Post a Comment Blogger Facebook
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.