Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ( Chadema) anayeshikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha Arusha Mjini amegoma kula kwa zaidi ya saa 48 sasa tangu alipokamatwa
Lema  alikamatwa juzi alfajiri akiwa nyumbani kwake Njiro Arusha kwa tuhuma  za kutoa maneno ya uchochezi  na kushawishi watu kwa njia ya mtandao  waandamane Septemba mosi.
Jana Meya wa Arusha, Calist Bukhay alisema Lema amegoma kula
Alisema  Lema aligoma kula akidai kuwa alifanyiwa udhalilishaji mbele ya watoto  wake wakati polisi walipokuwa wakitekeleza agizo la kumkamata.
"Ni  kweli amegoma kula tangu jana (juzi) alipokamatwa.Alisema askari polisi  walipkwenda kumkamata walimfanyia vitendo vya udhalilishaji mbele ya  watoto wake na kumnyanyasa bila kujali yeye ni kiongozi wa wananchi.
"Sasa   yeye ameshikilia msimamo wake kuwa kwa kuwa polisi walikuwa wamepanga  kumuua wakati wa kumkamata, basi ni bora akafa kwa njaa.

 
Post a Comment Blogger Facebook