Viongozi waandamizi wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana walikamatwa na Jeshi la Polisi wakati wakiwa katika kikao cha ndani katika Hoteli ya Giraffe mkoani Dar es Salam. 
Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.
Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.
Mwanasheria  Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwataja viongozi wengine waliokamatwa  kuwa ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji,  Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said  Issa.
Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao.
Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao.
Viongozi  hao walionekana wakiingia Polisi saa 10.30 jioni na kutoka saa 1.25  usiku, jambo ambalo liliwafanya wakae kituoni hapo kwa saa tatu. 
Lissu  alisema polisi walivamia kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 170,  wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama hicho na kuwakamata viongozi hao kwa  maelezo kuwa wamekaidi amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya  ndani na nje ya vyama vya siasa. 
Imeelezwa  kuwa viongozi hao wa Chadema walikuwa na mkutano uliotanguliwa na kikao  cha viongozi wakuu na kufuatiwa na cha viongozi hao kikijumuisha  wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri. 
Wakiwa  katika kikao hicho, ilielezwa kuwa watu wanne waliingia wakiwa  wamevalia kiraia na kuwaeleza kuwa viongozi wao wanahitajika kituo kikuu  cha polisi kutokana na kufanya mkutano kinyume cha sheria. 
Mbunge  wa Viti Maalumu, Upendo Peneza ambaye  alikuwa kwenye mkutano huo  alisema pamoja na mambo mengine ya chama, walikuwa wakijadili suala la  operesheni Ukuta la Septemba Mosi kama liendelee au lisiendelee kutokana  na hali ilivyo.
Kamanda  wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa  kuhusu kukamatwa kwao, alisema viongozi hao walikamatwa kwa kukukaidi amri ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ya kisiasa na kuchochea wananchi kuandamana kinyume cha sheria Septemba Mosi. 
Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo.
Wiki  iliyopita, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishana wa Operesheni na  Mafunzo, Nsato Marijani lilipiga marufuku mikutano ya ndani likisema  inatumika kuhamasisha watu kuvunja sheria za nchi na kupambana na  askari. Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo.
Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli za kisiasa hadi 2020.

 
Post a Comment Blogger Facebook