MWANAMKE  anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amekufa katika  mazingira yanayoonesha kwamba alibakwa kabla ya kuuawa na kutupwa  kichakani.
Mwili  wake ulionekana Agosti 10, mwaka huu saa 7.30 mchana katika Kijiji cha  Iringa Mvumi, Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.
Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kwamba wanamfanya  msako waliotenda unyama huo ili wawafikishe katika mkondo wa sheria.
Alitoa  mwito kwa wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi na vijiji vya jirani  kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wahalifu hao ili wachukuliwe  hatua za kisheria.
Wakati  huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma imemtupa jela  miaka 30 mkazi wa Kijiji cha Mlali Iyengu, Mkengela Mchechele (27) baada  ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 11.

 
Post a Comment Blogger Facebook