Mfalme  wa muziki wa taarabu mzee Yusuph maarufu kama "mfalme wa taarabu"  amefunguka na kusema kuwa sasa ameamua kuachana na muziki huo na  kumrudia Mungu huku akiwataka watanzania pia kumrudia Mungu.
Akiongea jana baada ya kumaliza swala ya Ijumaa kweneye msikiti wa Ilala Bungoni (Masjdi Taqwa) Mzee Yusuph alisema  kwa taarifa za awali watanzania wanatakiwa kutambua kuwa yeye ameachana  na muziki na sasa amemrudia Mungu na kuwataka kuwa na subira kwani  atatafuta siku maalum yeye kutangaza suala hilo ambapo atafunguka kwa  kirefu zaidi kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo.
"Ni  kweli nimeamua kuachana na muziki na sasa nimemrudia Mungu, nawaomba  watanzania wengine pia wamrudie Mungu, nitatafuta siku ambayo nitaongea  kwa kirefu zaidi juu ya suala hili, hivyo watanzania watambue tu  nimeachana na muziki sasa" alisema Mzee Yusuph.
Hii  ni mara ya pili kwa mzee Yusuph kutangaza kuacha muziki kwa mara ya  kwanza ilikuwa mwaka jana, alitangaza kuacha muziki na kuingia kwenye  siasa lakini hakuweza kufanya vizuri kwenye siasa na kurudi tena kwenye  muziki.

 
Post a Comment Blogger Facebook