0
Msanii mkongwe wa filamu, Jacob Stephen ‘JB’ amewataka mashabiki wake kuchangamkia shindano lake ambalo litawatoa washindi wawili ambao atakula nao chakula cha jioni katika moja ya hotel kubwa jijini Dar es saalam.
jb
Mwigizaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia filamu ‘Kalambati Lobo’ amesema ameshindwa kukaa na mashabiki wake wote na kuwashukuru ndo maana akanzisha shindano ambalo litampatia washindi wawili.
“Ndugu zangu najua mmekuwa mkini sapoti kwa nguvu zote na laiti ningekuwa na uwezo wa kuwafikia wote ningetamani siku moja tukae tuongee, tushauriane.” JB aliandika instagram. “Sasa kuelekea tarehe 29 mwezi wa 9 ambapo nitaachia movie hii ya Kalambati Lobo. Kesho nitatoa shindano dogo na washindi wawili nitakula nao chakula cha jioni kwenye moja ya hoteli kubwa, kama uko nje ya Dar nitagharamia usafiri wa ndege/basi pamoja na malazi. Nawapenda sana,”
Staa huyo wa filamu wiki chache zilizopita aliweka wazi mpango wake wa kuachana na kuigiza baada ya kuachia filamu zake mbili za mwisho.

Post a Comment Blogger

 
Top