0
Kocha wa klabu ya Stoke City Mark Hughes, amefunguliwa mashtaka na Chama cha soka nchini England (FA) kufuatia utiovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tottenham.
3829a8a800000578-0-image-a-52_1473713230745
Katika mchezo huo Stoke City walipoteza kwa kufungwa mabao manne kwa sifuri, Hughes alitakiwa kuondoka katika benchi la ufundi la Stoke City na mwamuzi Anthony Taylor, baada ya kutoa maneno makali anayodaiwa kuyatoa mbele ya mwamuzi namba nne, mara baada ya kikosi chake kufungwa bao la pili.
Licha ya kutoa maneno makali kwa mwamuzi huyo, Hughes pia anatuhumiwa kuvuka eneo lake la kutoa maelekezo kwa wachezaji, na alipewa onyo zaidi ya mara mbili.
Hughes ametakia kuwasilisha utetezi wa tuhuma zinazomkabili kabla ya siku ya ijumaa.
Stoke City ndo timu kwa ambayo kwasasa inaburuza mkia wa msimamo wa ligi ya nchini England (PL) msimu wa 2016/17, ikiwa imejikusanyia point moja iliyo pata katika mchezo dhidi ya Middlesbrough

Post a Comment Blogger

 
Top