0
Rapper Nikki Mbishi amefunguka kuhusu wimbo wake ujao, ‘Babu Talent’ ambao anadaiwa kumuimba Babutale kwa asilimia 100.
nikki
Akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV, rapper huyo amedai kuwa wimbo huo unaweza ukamgusa meneja huyo wa Diamond kwa asilimia ambazo yeye mwenyewe anazoweza kuzihisi.
“Yeye ni mwenye muziki kwahiyo?,” aliuliza Nikki. “Wamejiongeza wao, ni sawa sawa na kumuimba Nay Wa Mitego, mimi nilimuimbia mwanamke sasa nyinyi mnamjua Nay Wa Mitego huyo ni wa kwenu nyie.”
“Ngoma very soon inakuja watu wakae tayari sasa hivi kwa maandalizi kwa sababu nafanya version za Babu Talent tofauti tofauti. Kuna moja imeshafanyika kuna nyingine bado session zipo kwa sababu watu wengi wameniomba kuniofa mdundo wa kufanya hiyo kitu,” aliongeza

Post a Comment Blogger

 
Top