Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya kwanza ( kama hukuisoma bofya hapa)
 
Sehemu ya pili
Ilipoishia sehemu ya kwanza ( kama hukuisoma bofya hapa)
.....Wakati  wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa  uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....  
Sehemu ya pili
...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. 
Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti Kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka.
  
"Nenda  mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa  amelinyanyua karatasi like kwa mkono wake wa kushoto. Karatasi  likatoweka mkononi mwake na kupepea kwa nguvu kama vile limerushwa na  upepo mkali.
Doreen  alipomaliza kazi hiyo akasimama vizuri kama mwanajeshi aliyejipanga  kwaajili ya gwaride kisha akainamisha kichwa chake chini akapotea eneo  lile.
**********
Wanafunzi  wa shule ya sekondari Mabango walikuwa wanahofu kubwa sana kila wakikaa  walifikiria kifo tu. Usingizi haukuwajia hata Mara moja hivyo usiku  waliketi makundi makundi wakizungumza hili na lile.
Wakati  huo Dorice rafiki kipenzi wa Doreen alikuwa amejitenga pembeni  akizungumza na mpenzi wake aitwaye Eddy, kijana mtanashati, mzuri, mpole  na akili nyingi sana darasani.Wasichana wengi shuleni pale walitamani  kuwa nae lakini bahati ilimwangukia Dorice pekee.
  
"Eddy  unajua naogopa sana.." ilikuwa sauti ya Dorice akiwa amemkumbatia Eddy  kwani kigiza kile cha usiku kiliwaficha wasionekane hivyo wakajiachia.
"unaogopa nini Dorice mpenzi wangu?"
"Naogopa kufa!" binti Huyo wa kinyaturu, mrembo aliyeumbika aliongea kwa sauti ya madeko sana.
"siku  zote nakwambia Dorice kama Mungu alipanga huwezi kupangua , mwanadamu  asikutishe kwa lolote. Huyu anayeua wenzake naye IPO Siku yake tu!"
"Najua baby Ila hali inatisha"
"Tuzidi kuomba Mungu mpenzi wangu kila unalofanya muombe Mungu."
"Nakupenda "
"Nakupenda pia"
Wakati Eddy na Dorice wakiendelea kuzungumza maneno hayo, Doreen alikuwa nyuma ya mti waliosimama hivyo alisikia kila kitu. 
Roho ilimuuma sana kwani tangu alipohamia shuleni hapo alitokea kumpenda sana Eddy na alitamani awe mpenzi wake kwani ndio chaguo la moyo wake lakini Dorice alikuwa kikwazo. .
Suala hilo lilimuumiza Doreen ndani kwa ndani. Akainuka pale kwenye mti na kupita katikati yao, akamwita Dorice pembeni.

"Dorice.. mimi nawahi kulala Ila kesho unione!"
"nikuone?"
"ndio  kwani hujaelewa?" alijibu Doreen kwa ukali jambo lililomwachia maswali  mengi Dorice. Lakini Doreen hakujali kitu akaondoka zake Ila moyoni  alipanga jambo zito la kumfanyia Dorice siku ya kesho yake.
*********
Ilikuwa asubuhi tulivu sana majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ambapo mwalimu Dayana Mbeshi aliwahi ofisini kwake kama ilivyokuwa kawaida yake. 
Majengo ya ofisi yalimkaribisha kwa shangwe naye akaitikia ukaribisho huo kwa kufungua ofisi yake kisha akasogeza mapazia ya dirishani ili kuruhusu mwangaza wa jua changa uweze kupenyeza vizuri.
Baada ya kukamilisha yote hayo Madam Mbeshi akasogeza kiti chake karibu na meza kisha akaketi halafu akaanza kusogeza vitu vilivyokuwepo mezani pale lakini ghafla akakutana na karatasi chafuchafu mezani kwake lakini ilikuwa na maandishi.
Akashtuka kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao...............

Post a Comment Blogger Facebook