MTUNZI:ENEA FAIDY
Ilikuwa  ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa  ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo  ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi  na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu.
Mkuu  wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini  chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa  ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na USO  wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule
"vipi kulikoni?"
"hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu.
"what?  mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku  akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake.
******
Wanafunzi  wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi  kutokea katika shule yao. Kila MTU aliwaza sana juu ya vifo vile huku  kila mmoja akihisi zamu yake IPO karibu. Nyuso za huzuni ndizo  zilizotawala kwa wanafunzi wote si wa kike  wala wa kiume. Hakuna aliyetamani kulala wala kukaa mbali na kundi la  watu kwani hofu iliwajaa mioyoni mwao, hawakuweza hata kusoma.
Lakini  hali ilikuwa tofauti sana kwa binti Doreen ambaye alikuwa na wiki tu  toka ahamie shuleni hapo. Alionekana kutoogopa chochote wala kuguswa na  misiba ya wanafunzi  wenzake. Kila Mara alionekana akiwa na furaha, hali hii iliwatisha  wanafunzi wenzake na kuwafanya wawe na maswali mengi juu yake. 
Doreen alikuwa msichana mrembo, sura yake  nyembamba iliyopambwa na macho makubwa legevu, kope ndefu nyeusi tii,  pua nyembamba iliyochongoka vyema na midomo mizuri yenye mvuto wa aina yake vilimfanya awe tishio kila kona kwani alikuwa ni mzuri kupindukia lakini Tabia  ilikuwa tofauti na uzuri wake.
Wakati  wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke  take nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa  uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....  
Itaendelea.......
Itaendelea.......

 
Post a Comment Blogger Facebook