ILIPOISHIA
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar  aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda  kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzi vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi  wake analo lihitaji
ENDELEA 
“Habari yako dada?”
Kijana  wa Muntar alimsalima Agnes ambaya kwa haraka akaliachia tabasamu lake  mdomoni na kuufanya uso wake kuzidi kunawiri kwa uzuri
  
“Salama mamo vipi?” Agnes alizungumza kwa sauti nyororo ya kuvutia hadi muhudumu kiume wa vinywaji akaguna
“Salama.....kwa jina mimi ninaitwa Kibopa na yule pale alavalia cheni nyingi ni bosi wangu anaitwa Muntari”
“Aahaa nashukuru kuwafahamu,Samahani kaka ninaomba unipatie Red’s mbili za baridi kiasi”
“Muhudumu mpe katon nzima pesa nitalipa mimi?”
“Jamani kaka yangu mimi sio mnywaji sana”
“Ahaa usijali nyingine unaweza kunywa leo au hata kesho”
“Asante sana”
  
Muhudumu akamkabidhi Agnes katoni ya kinywaji alicho muagizia na kibopa akatoa pesa na kumlipia muhudumu.
“Sasa sister kama huto jali ninaomba namba yako ya simu”
Agnes bila wasiwasi akamtajia Kibopa namba yake ya simu,wakaagana ana Agnes akarudi sehemu alipo Rahab
“Jamaa ameshaingia mkenge sasa kazi ni moja sawa”
“Hapo ndipo ninakupendea Ag”
“Chezea mimi wewe,kumbe mtu ukiwa na kalio kubwa nalo linasaidia”
Wakacheka  na kufungua vinywaji na kuanza kunywa taratibu.Muntar akakabidhiwa  namba na Kibopa na akaipiga na Agenes akaipokea na kama kawaida na sauti  yake nyororo aliyobarikiwa kutoka mbinguni akazungumza
“Nani mwenzangu?”
“Ukigeuka upande wako wa kushoto utaniona nimevaa shati jeupe na cheni za dhahabu”
Agnes akageuka na kumfanya Muntar kupunga mkono akimuashiria kuwa ni yeye ndiye aliye mpigia simu
“Mrembo nakuomba basi uje kujumuika name hapa?”
“Naona aibu labda nije na mwezangu”
“Hilo tuu hakuna tatizo ni wewe tuu”
“Sawa ninakuja”
  
Agnes  akakata simu na kumtazama Rahab kwa pamoja wakatabasamu na wakasimama  na kuanza kutembea kwa mwendo wa maringo na kupishwaviti na wapambe wa  Muntar kisha wakakaa
                                                                       ***
Dokta  Wiliama akawashusha kwenye gari Anna,Halima na Fety mbali kidogo na  hotel ya Serena huku kila mmoja simu yake ikiwa na salio la kutosha  pamoja na picha ya Karim Yussuf kijana mwenye umri mdogo ila anasifika  sana kuwa na utajiri mkubwa kutokana na Sheli za mafuta anazo zimiliki  kila kona ya mikoa ya Tanzania.Kila mmoja akaingia Hotelini kwa muda  wake na kuelekea kuketi katika upande wake ila kwa pamoja wakawa na  mawasiliano ya ujumbe mfupi wa meseji.Kutokana ni muda wa jioni hawakuwa  na papara kwani watu wengi bado hawakuwa wameingia Hotelini kuendelea  na starehe zao.Macho ya Fety yakatua kwa jamaa anayeingia kwenye  mlango  wa kuingilia akiwa ameongozana na mwanamke mrembo
{Nimemuona}
  
Fety  akausamba ujumbe kwa wezake ambao wapo maeneo ya tofauti kwenye hoteli  na taratibu simu yake akaichomeka kwenye suruali yake na kuendelea  kumtazama Karim ambaye moja kwa moja aka anaelekea sehemu yenye milango  ya lifti zinazo kwenda juu  na kushuka chini,Kutokan-a na Lifti kutumika  ikamlazimu Karimu na mpenzi wake kusimama kwa muda kuzisubiria.Kwa  haraka Fety akasimama na kupiga hatua za haraka kabla hajafika sehemu  alipo Karimu,lifti ambayo wanaisubiria ikafunguaka,Karim na mpenzi wake  wakingia ila kabla haijajifunga Fety akawahi kuizuia na kuingia
“Habari zenu?”
“Salma”
  
Karimu  kutokana na kutokuwa na aibu akaanza kumshika shika mpenzi wake na  kuchezeana katika sehemu zao nyeti.Mcho ya Fety yakawangalia kwa umakini  kisha akayahamishia masho yake kwenye kamera mbili za ulinzi zilizopo  ndani ya lifti kabla hajafanya kitu chochote akastukia lifti ikisimama  hii ni baada ya mpenzi wa Karimu kuminya kitufe cha kuisimamisha  lifti.Kufuma na kufumbua Fety akastukia ngumi kutoka kwa mpenzi wa Karim  ikitua kwenye shavu lake na kumsfanya kuweweseka kasha akaanza kuikwepa  mikono inayoimjia mwilini mwake kutoka kwa Karimu na mpenzi wake Shamsa  mwenye asili ya kiarabu.
                                                                           **
Karimu  na Shamsa wanaasili ya Oman japo wanauraia wa nchi zote mbili Tanzania  na Oman,japo watu wengi waliwaona machoni mwao wanadhani ni watu wema  hii ni kutokana na jinsi wanavyo jitoa katika shughuli mbali mbali za  kijamii na mara nyingi huwa wanawasaidia wasio jiweza kila siku ya  Ijumaa na jumamosi nje ya jumba lao lililopo maeneo ya Mbezi beach.Japo  wanautajri mkubwa wa magari ya kifahari,masheli,maduka na mahoteli ya  kifahari ila  bado hawaridhiki na utajiri huo na wanaendelea kufanya  kazi za haramu ili kuzidi kuuongeza utajiri mara dufu.Jambo la kuua kwao  ni sawa na mtu kumchinja kuku siku ya sikuku.
  
Hadi  wakati huu Serikali ya Tanzania inashindwa kutambua ni jinsi gani  wanaweza kuwatia nguvuni Karimu na mpenzi wake wakiwa katika  kidhibitisho kitakacho wawezesha kuwastaki katika mahakama kuu ya  Tanzania na kuwatupilia jela.Kila mbinu ambazo serikali waliitumia  wakajikuta wakishindwa hii ni baadhi ya viongozi wasio waaminifu  kuwapenyezea siri Karim na Shamsa  na hujipanga upya katika kuwatoroka  askari.
Amri ya kuwaua watu waote wanaoshindikana kukamatika na kirahisi ilitolewa ma raisi tena kwa siri kubwa na watu walio husishwa katika kazi hiyo ni Dokta William na Mkuu mstaafu wa jeshi bwana Clinton Tony ambao wote ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa raisi na mara nyingi humshauri riasi katika maswala mengi ya kukabiliana na ugaidi hii ni kutokana na ujuzi wao katika maswala ya kigaidi
  
Amri ya kuwaua watu waote wanaoshindikana kukamatika na kirahisi ilitolewa ma raisi tena kwa siri kubwa na watu walio husishwa katika kazi hiyo ni Dokta William na Mkuu mstaafu wa jeshi bwana Clinton Tony ambao wote ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa raisi na mara nyingi humshauri riasi katika maswala mengi ya kukabiliana na ugaidi hii ni kutokana na ujuzi wao katika maswala ya kigaidi
Pasipo  wao kujua Agnes,Anna,Rahab,Fetty na Halima wanatumiwa na serikali  kisiri na kwaimani yao wanatambua kuwa mtu anaye waagiza kazi hiyo ni  dokta Williama ambaye amewafundisha mbinu nyingi za kigadi ili kupambana  na magaidi wanao itesa serikali ya Tanzania pamoja na jeshi la polisi.
  
***********
Fetty  anajipanga vizuri na kuanza kupambana nao kufa na kupona kutokana na  ujuzi mkubwa wa kukabiliana na adui anafanikiwa kumpiga Shamsa ngumi  kadhaa sehemu ya shingo na kumfanya apate wenge linalo mkalisha chini  huku machoni mwake akiona nyota nyota nyingi.Karimu anashangaa kukutana  na msichana jasiri anaye vumilia makonde ya mazito kutoka kwake na kwa  haraka anamisha kitufe na lifti inaanza kwenda juu huku akiendelelea  kuyapangua mateke ya Fetty kwa kutimia mikono yake iliyo komaa.
Lifti inafunguka gorofa ya tano na Karimu anajirusha nje kabla Fetty hajapiga hatua anastukia akishikwa mguu na kuvutwa chini na Shamsa na kuangukia uso na kumshuhudia Karimu akichanganya miguu kwa kasi kubwa na kupolelea anapo pajua mwenyewe.Shamsa akamkalia kwa haraka Fetty mongoni na kuanza kumvuta nywele huku akijaribu kukipigisha kichwa cha Fetty chini.Kwa nguvu zake zote Fetty akajikaza mwili wake kuanzia juu hadi chini na kujinyanyua kwa nguvu hadi akasimama ila Shamsa akaendelea kumng’angania mgongoni huku mkono wake ukiwa umeikaba kwa nguvu zake zote shingo ya Fetty.
Lifti inafunguka gorofa ya tano na Karimu anajirusha nje kabla Fetty hajapiga hatua anastukia akishikwa mguu na kuvutwa chini na Shamsa na kuangukia uso na kumshuhudia Karimu akichanganya miguu kwa kasi kubwa na kupolelea anapo pajua mwenyewe.Shamsa akamkalia kwa haraka Fetty mongoni na kuanza kumvuta nywele huku akijaribu kukipigisha kichwa cha Fetty chini.Kwa nguvu zake zote Fetty akajikaza mwili wake kuanzia juu hadi chini na kujinyanyua kwa nguvu hadi akasimama ila Shamsa akaendelea kumng’angania mgongoni huku mkono wake ukiwa umeikaba kwa nguvu zake zote shingo ya Fetty.
                                                                                   ***
Simu  za Fetty,Halima na Anna zina Software ambayo kila mmoja wao anapo  kwenda ni lazima simu zao ziingize ujumbe katika simu za wezao kuwa ni  sehemu gani alipo mmoja wao.Anna akampigia simu Halima na kumpa taarifa  Anna wakutate katika milango ya kiingilia kwenye lifti
“Anna,Fety  yupo kwenye matatizo ninavyohisi kama unaweza kuiona simu yako  inavyoonyesha kuwa yupo eneo maoja  tuu kwa zaidi ya dakika kumi sasa”
“Location inaonyesha yupo gorofa namba tano”
“Sasa tujigawe,wewe pita kwenye ngazi na mimi nitumie lifti”
“Sawa”
  
Halima  akaingia kwenye lifti na kuminya kitufe cha gorofa ya tano,huku alima  naye akaanza kuzipandisha ngazi kwa haraka kuelekea juu gorofa ya tano  japo ni ndefi ila akajikata kutembea kwa mwendo wa kukimbia
  
                                                                                     ***
Kwa  haraka wazo lililo mjia Karimu ni kushuka kwa kupitia ngazi kuepukana  na kukutana na Fetty ambaye tayari alisha mzidi ujanja na maarifa ya  kila aina.Karimu akaanza kushusha kwenye ngazi huku akikimbia na  kutazama tazama juu kama Fetty akamfwata ajue ni jinsi gani ya kuongeza  juhudi za kukimbia.Macho ya Anna yakamshuhudia jinsi Karimu anavyoshuka  kwa kasi huku hasho jingi  likimwagika na shati lake likiwa limejikunja  kunja kama limetafunwa na ng’ombe mwenye njaa kali,Anna akapunguza  mwendo na hadi Karimu anamfikia kwa ustadi mkubwa wa hali ya juu  akampiga teke la miguu Karimu na kumfanya aanguke vibaya na kuanza  kubingiria kwenye ngazi akielekaea chini akitoa kelele kali za vilio.
  
                                                                          ***
Fetty  akaanza kuishiwa na pumzi mwilini mwake kutokana na kabali takatifu  aaliyo pigwa na Shamsa msichana ambeye kwenye maeneo mazima ya kupiga  anayapenda tangu akiwa mtoto mdogo wa miaka mitano.Fetty kila alipo  jaribu kuitoa mikono ya Shamsa akajikuta akishindwa kwani Shamsa  anahakikisha kuwa anaondoka na roho ya Fetty,taratibu Fetty akaanza  kushuka chini huku jicho likiwa linaanza kumtoka akimshuhudia mtoa roo  akiinyemelea roho yake.Mlango wa lift aliyo panda Halima ukafunguka na  akatoka nje akatazama pande zote za kardo akaona hakuna dalili yoyote na  mtu,Akasikia kishindo na kukuroma kwa mtu kwenye mlango wa pili wa  lifti ambao unshindwa kujifunga kutokana na kiatu chekundu lilicho zuia  katikati na kuifanya milango hiyo kujisogeza na kurudi inapotoka.Halima  akamshuhudia Fatty akilazwa chini na msichana anaye miminika kwa jasho  jingi japo ndani ya lifti hii kuna hewa ya kutengenezwa AC(air condion)
  
Halima  hakupoteza muda,akaingia na kuzishika nywele za Shamsa na kumvuta nje  kwa nguvu zake nje na kumfanya Shamsa kuburuzika kwenye sakafu  iliyotengenezwa vizuri na kufanania na kioo.Akamgauza Faetty na kumkuta  akikohoa kohoa akiyaruhusu mapafu yake kuingiza hewa ya kutosha.Shamsa  akasimama na kuanza kukimbia kujiokoa maisha yake
“A....nak....imbi....a.”
Fetty alizungumza kwa shida huku mkono wake mmoja akimnyooshea Shmsa anayechanja mbuga
“Upo vizuri lakini?”
“Nd...io muwah....i anatoroka”
  
Halima  akamtazama vizuri Fetty na kuridhishwa na afya yake na akasimama kwa  haraka na kuanza kumkimbiza Shamsa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya  kukimbilia zaidi ya kujirusha kwenye mlango mmoja uliopo mbele yake na  kwabahati nzuri mtu aliyopo ndani ya chumba hicho ndio alikuwa  ameufungua na kukishika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kutoka nje.
Kikumbo cha Shamsa kikamfanya mwenye chumba kuanguka chini pamoja na simu yake ambayo alikuwa anasoma meseji iliyomfanya asimame kwenye mlango huku akiwa ameshika kitasa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya bafuni ambapo Halima naye akaingia na kwa haraka Shamsa akachukua kibakuli chenye sabuni ya unga na kumbwagia Halima ya uso
Kikumbo cha Shamsa kikamfanya mwenye chumba kuanguka chini pamoja na simu yake ambayo alikuwa anasoma meseji iliyomfanya asimame kwenye mlango huku akiwa ameshika kitasa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya bafuni ambapo Halima naye akaingia na kwa haraka Shamsa akachukua kibakuli chenye sabuni ya unga na kumbwagia Halima ya uso
                                                                             ***
Muntar na watu wake wakazidi kunywa pombe na kuwaomba Agnes na Rahabu wawe wageni wao kwa usiku wa leo.
“Jamani  sisi hatuhitaji kulala kwenye hoteli hii.” Agnes alizungumza huku  akikichezea kifua cha Muntar ambaye muda wote anakazi ya kutabasamu  tabasamu
“Nyinyi mutanata wapi watoto wazuri?”
“Hoteli yoyote ila si hapa”
“Wee kibopa fanya mpango wa kutafuta vyumba vya mjini kwenye hoteli nzuri nzuri unazo zijua”
“Bosi hotel ambayo ipo powa kwa haraka haraka ninaona ni Mtendele”
“Ipo wapi hiyo?”
“Maeneo ya Chuda raha”
“Sawa twendeni”
  
Wakasimama  na wote wakatoka nje,Rahabu na Agnes wakaingia kwenye gari lao na  Muntar na wapambe wake wakingia kwenye gari yao aina ya HAICE na  taratibu wakaanza safari ya kuelekea katika Hotel ya Mtendele
“Ag hawa watu tunawaua kwa nama gani?”
“Una maana gani?”
“Namaanisha kwa kuwanyonga au kwa kuwapiga risasi?”
“Lengo letu sisi ni huyo Muntar hao wengine tuwapotezee”
“Huoni watakuwa ni watu wa kwanza katika kutusaka sisi?”
“Sawa ila tutajua ni jinsi gani ya kuwaua endepo nao wataingia kwenye kumi na nane zetu”
“Powa hii ishu tuifanye usiku huu huu na turudi zetu kambini”
  
“Powa ni wewe tuu kikubwa ni umakini na hiyo bastola yako ikoki tayari kwa mashambulizi”
                                                                 ***
Muntar na wapambe wake wanaendelea kuburudika na mziki gafla Muntar akazima redio ya gari na kuwafanya wapambe wake kumtazama
“Sikilizeni nyinyi....mpango wetu ni kama munavyo ujua,Sisi mwanamke kwetu ni begi la safari na hawa pia iwe hiyo hivyo”
“Sawa bosi ila mimi sijaelewa kidogo hapo kwa maana hawa nao pia tunatakiwa kuwaua?”
“Ndio ni lazima wafe”
“Ahaaa bosi huoni maduu wazuri kama hawa pia tuwauee ,Acha basi tuspend nao kama siku mbili tatu nne hivi”
Kwa haraka Muntar akachomoa bastola yeka na kumelekezea Kibopa ambaye muda mwingi anapenda sana wasichana wazuri
  
“Katika  wakati wa kazi huwa sipendi masihara.....na ole wenu miongoni mwenu  nione mtu anajipendekeza kwa msichana yoyote nitamtoa roho,Tuna wakamata  na kuwachinja na ndani ya matumbo yao tunadumbukiza shehena yote ya  madawa ya kulevya tuliyo nayo.SAWA?”
“Sawa bosi’
Wote  wakaitikia kwa woga huku Kibopa mwili wake wote ukiwa unamtetemeka  kwani Muntar ni mwanaume asiye na huruma kwa mtu wa aina yoyote katika  swala zima la biashara zake haramu.Usemi wake mkubwa ni bora punda afe  ili mzigo ufike
SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……4
Kwa  bahati mbaya katika maeneo ya barabara ya Railys,wakakuta ajali  ya  daladala iliyosababisha magari mengi kusimama kwa muda,Kutokana hawakuwa  na haraka ikawalazimu kupanga foleni na kuwaacha askari wa usalama  barabarani kumaiza vipimbo vyao.
“Rahab nahisi kuna kitu kwenye gari la kina Muntar.” Agnes alimuambia Rahabu
“Kitu gani?”
  
“Kama  wanakitu wanakijadili na ona oana jinsi Muntar anavyo zungumza huku  akiichezesha chezasha mkono wake ulioshika bastola?” Agens alimuonyesha  Rahab na kwakusaidiwa na mwanga wa taa za magari mengine waliweza  kuliona tukio la ndani ya gari
Rahab akaitoa bastola yake na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti,akataka kushuka kwenye gari ila Agnes akamzuia
  
“Mbona unakuwa kama mjinga unataka kwenda wapi?”
“Tuwafyatue tusepe zetu”
“Huoni hao askari hapo au unataka tukimbizane kimbizane?”
Wote wakajikuta macho yao yakimsindikiza askari anaye gongwa kwenye kioo cha gari walilomo Muntar na watu wake
  
                                                      ***
Muntar akamtazama askari anaye gonga kioo cha gari lao,Akaitazama astola yake na kukishusha kioo taratibu
“Shukeni  ndani ya gari.” Askari aliwaamrisha na kuwamfaya Muntar kufyatua risasi  mbili kwa haraka,milio ya risasi ikawafanya watu waliopo kwenye eneo  kuanza kutawanyika kuokoa maisha yao.Askari wengine watatu waliopo  katika eneo la tukio wakajibanza kwenye magari mengine wakiwa na bunduki  zako na kuanza kujibu mashambulizi kuelekea kwenye gari la Muntar
  
“Rudisha nyuma gai hilo.”
Muntar  alimuamuru dereva wake na akatii,Wakaligonga gari walilomo Agnes na  Rahab na kulifanya lirudi nyuma na kuyagonga magari yaliyopo nyuma  yetu.Rahab akaanza akaanza kufyatua risasi katika matairi ya gari la  Muntar na kulifanya lipoteze muoelekeo hii ni baada ya breki za gari lao  kushindwa kukamata vizuri na kugonga kwenye vyuma vya reli.Watu wa  Muntari,mmoja baada ya mwengine wakaanza kujirusha nje ya gari wakiwa na  bunduki zao aina ya ‘Short gun’ na kuendelea kufanya mashambuliza kwa  askari.
  
Agnes  akafungua mlango wa gari lao na kupiga goti moja chini,Bastola yake  ikawa na kazi mija tuu ambayo ni kufyatua risasi kwa kila mtu wa  Muntar.Muntar akazidi kuchanganyikiwa baada ya watu wake kuwaona wakiwa  wanaanguka mmoja baada ya mwengine.Hadi akabaki akiwa na Kibopa ambaye  wakati wote wezake wakipambana yeye alikuwa na kazi ya kujibanza kwenye  gari lao
  
Muntar  akaona nafasi pekee ni kukimbia,kwa bahati nzuri pembeni kuna pikipiki  iliyo acha na raia aliyekuwa akijiokoa maisha yake kwa kuiamini sana  miguu yake kuliko pikipiki.Akapanda na Kibopa akadanda kwa nyuma  wakaondoka kwa kasi wakikatiza katokati ya njia za reli.
  
Agnes  na Rahab wakaingia ndani ya gari,Agnes akalirudisha gari lao nyuma na  kupata upenyo wa kuiwezesha gari yao kupita na kupita njia ambayo Muntar  amekimbilia.Askari wakashindwa kufyatua risasi kwatika gari linalo  wafukuzia majambazi kwani hawakujua walio wasaidia ni kina nani.
  
Muntar  akazidi kukanyaga mafuta na kuingia barabara inayokwenda mikoani  akikatiza katika kiplefti cha kwaminchi,Agnes akawa na gazi ya kupiga  honi akiashiria watu waliopo barabarani kuwapiasha.Akazidi kukanyaga  mafuta kwa kasi huku akiikaribia pikipiki ya Muntar.Kibopa akaanza  kufyatu risasi kuelekea lilipi gari walilopo Agens.
  
“Shiti....”  Rahab alizungumza huku akinang’ata meno yake,alikataka kujitokeza  kwenye kioo cha gari ila akarudi ndani kwa haraka baada ya kioo kidogo  cha pembeni kuvunjwa kwa risasi anazo zipiga Kibopa pasipo kuwa na  utaratibu wowote.Gafla kibopa akalikwepa Scania linalo toka kwenye  kiwanda cha unga Pembe maeneo ya Kange na karibia robo mbili ya gari  imeziba barabara na kuachanisha uwazi mdogo unao weza kuiruhusu pikipiki  kupi na kuendelea mbele kwa kasi.Agnes akafunga breki za gari lake kwa  kasi na kuiingiza upande wa kulia kwake kukikwepa kichwa cha gari kubwa  la unga,Gari karerereka pembeni ya barabara na kwakusadiana na Rahab  wakaushika mskani wa gari na kuurudisha upande wa kulia 
  
Gari  ikakaa sawa barabarani,kutokana na mstuko katika injini,gari ikazima  katikati ya barabara na milago yote kujifunga.Kwa kutumia vitako vya  bastola zao wakapasua vioo vya madirisha ya magari na kujitoa ndani ya  gari lao,linalo toa mlio wa kuashiria linaitilafu sehemu
“R...itakuwaje sasa?”
“Ndio hivyo jamaa wamesha sepa.”
“Ngoja kwanza.” Agnes akaenda eneo lenye maegesho ya boda boda(waendesha pikipiki),
“Ni kina nani wanaweza kuendesha pikipiki kwa kasi kubbwa?”
  
Kila muendesha pikipiki akaa kimya huku macho yao wakiitazama bastola ya Agnes.
“Ohoo nahisi munaiogopa hii bastola? Mimi ni raia mwema ninaomba masaada wa kuwakimbiza wale watu walio pita hapa?”
”Dada  mimi piki piki yangu haina mafuta?” Jamaa mmoja alizungumza huku  akilivua kofia lake,wengine wote wakakataa.Rahab akafika eneo alipo  Agnes
“Ag wanasemaje?”
“Hawataki?”
  
Rahab  akapiga risasi moja hewani,kila dereva aliye ipenda rogo yake akaaruka  kwenye pikipiki yake na kuchanganya kwato zake kuooa maisha yake.Rahabu  akapanda kwenye moja ya piki piki aina ya Boxer,ambayo dereva wake  aliisahau funguo yeke.Muntar kadri anavyozidi kuendesha pikipiki ndivyo  jinsi mafuta yaliyozidi kuteketea,na taratibu piki piki ikaanza kugoma  na mwisho wa siku ikagoma kabisa hata kusogea hatua mbele.Rahab akazidi  kuvuta mafuta ya pikipiki waliyo panda,kwa mbali wakawaoana Muntari na  Kibopa wakishuka kwenye pikipiki yao na kuinga pori.
  
                                                                                     ***
Shamsa  baada ya kumuona Halima anaanza kuhangaika kwa sabuni ya unga aliyo  mwagia usoni,kwa haraka akafungu mlango wa chumba na kuaanza kukimbia  kuelekea zilipo ngazi za kushuka.
  
Anna  kwa haraka akashuka kwenye ngazi na kuanza kumshindilia mateke Karim  ambaye amechoka kwa kiasi kikubwa sana.Karim akajihahidi kujiinua ila  Anna akawa makini kwa kila jambo na kwa haraka akaiwahi shingo ya Karimu  na kuizungusha kwa nguvu na kuivunja.Kitendo cha Karimu kuuawa  kikashuhudiwa na Shamsa ambaye ndio yupo kwenye harakati za kujiokoa  kutoka mikononi mwa Halima.
  
Anna  hakumjali Shamsa ambaye amesimama kwa mshangao akiwa haamini kwa kitu  kilicho tokea kwa mpenzi wake anaye mpenda kuliko kitu cha aina  yoyote.Kwa haraka Shamsa akashuka kwenye ngazi kwa hasira na kumrukia  Anna ambaye akajibamiza kwenye ukuta,Shemsa akajaribu kumrukia Anna  ambaye alifanikiwa kumkwepa na kwa bahati mbaya Anna akamsukuma Shamsa  ambaye akaanza kwenda chini kutoka gorofa ya nne hadi kwenye sakafu na  kichwa chake kikapiga chini na kikapasuka mbele ya macho ya polisi na  baadhi ya wateja wengine
  
Anna  taratibu akapiga hatua na kuchungulia sehemu aliyo angukia macho yake  yakakutana na askari tishio ambaye ni mpelelezi wa kutegemewa nchini  bwana Jackson Luther
  
                                                                                      ***
Rahab  anazidi kuvuta mafuta ya pikipiki hadi kwenye njia walio ingilia Muntar  na KIbopa mbao walizidi kuongeza mwendo wa kukimbia baada ya kuiona  pikipiki ikiwafwata kwa kasi nyuma yao.Kwa bahati mbaya Muntar  na   Kibopa waliishiwa risasi katika silaha zao,kila mmoja akakimbia kwa  upande wake anao ujua yeye ili kutaokoa maisha yake,Rahabu akapunguza  mwendo wa pikiki na Agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda  Kibopa,Rahab akapita njia aliyo kwenda Muntar.
Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla Rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na Muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi
Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla Rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na Muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi

 
Post a Comment Blogger Facebook