0
Wakuu wa ndondi wamesitisha kibali cha bondia Tyson Fury kupigana ikiwa ni siku moja baada ya bondia huyo kusalimisha mataji yake ya ubingwa wa ndondi uzani mzito duniani ili kuweza kukabiliana na matatizo ya afya ya akili.
_91911739_f18173f8-0bab-4e44-8f49-85156b31bcf1
Fury, ambaye ana umri wa miaka 28, hajapigana tangu alivyo mshinda Wladimir Klitschko mnamo Novemba 2015 na amesusia mechi mbili za marudio.
Bodi ya udhibiti wa mchezo wa ndondi Uingereza – British Boxing Board of Control – imethibitisha kuwa kibali chake kimesitishwa kwa muda “ikisubiriwa uchunguzi wa ziada dhidi ya tuhuma za utumiaji madawa ya kusisimua misuli na masuala ya afya”.
Fury alishtakiwa kwa makosa ya kutumia dawa za kusisimuwa misuli na taasisi ya Uingireza ya kupambana na madawa hayo mnamo mwezi Juni.
Jumatano Fury alisalimisha mataji yake ya ubingwa wa ndondi uzani mzito WBO na WBA, akieleza kuwa hawezi kuyatetea mataji hayo kutokana na afya yake.
Inambidi sasa akutane na bodi hiyo ya ndondi Uingereza kabla ya kufikiwa uamuzi kuhusu iwapo atapigana tena au la.
Rufaa aliokata katika kesi ya utumiaji wa dawa za kusisimua misuli inatarajiwa kusikilizwa Novemba.
Mapema mwezi huu, Fury alionekana kutangaza kustaafu kwake katika mtandao wa Twitter, kabla ya kujitokeza saa chache baadaye kukiuka kauli hiyo , na kufichua katika mahojiano na jarida la Rolling Stone kwamba anatumia mihadarati kumsaidia kukabiliana na msongo wa mawazo.
Source: BBC

Post a Comment Blogger

 
Top