ROHO MKONONI 02 0 HADITHI, za kusisimua 10:22:00 PM

MTUNZI: George Iron Mosenya

SEHEMU YA PILI

"Kama shilingi 5000 ya imetushnda itakuwa 30000?" alijiuliza baba Joyce huku akisimama na kutoka nje ambapo aliwakuta Betty na Joyce. Hakuwa hata na la kusema zaidi ya kuwakodolea macho yaliyokata tamaa kabisa.
"Basi mimi nina damu ya kundi 'O' niruhusu nitoe" alisema Joyce kwaq kiherehere akikumbuka majibu aliyopewa juu ya kundi la damu yake siku alipojitolea damu, jambo ambalo mzazi wake alipinga vikali kwa kuhofia usalama wa mwanae huyo mkubwa kutokana na umri wake kuwa mdogo..
Mgogoro ukaanzia hapa na kusafiri hadi nyumbani, wazazi wakipingana na Joyce. Joyce akisimamia msimamo kuwa anaweza kutoa damu na kumwokoa mama yake Betty….
Huu ukawa utata ulioishia katika mtafaruku, Joyce akakimbia na baiskeli akiwaacha mama na kaka yake wakitukanwa……
Akakimbilia alikotambua yeye na akili yake……

BETTY ni kama alikuwa amekata tamaa tayari, hakuna aliyemtegemea zaidi ya sala zake zisizokuwa na imani ndani yake. Anakumbuka aliwahi kumwombea baba yake aliyekuwa mahututi lakini bado alikufa. Sasa ni mama yake. Betty akajitayarisha kuwa yatima na bado huo utayari hakuuona kama unawezekana. Ataishi vipi sasa? Bila mama na baba…..
Ulikuwa mtihani mkubwa kuliko…..daktari alingojea mama Betty avute pumzi ya mwisho, mwili ukabidhiwe kwa ndugu zake kisha ukafukiwe ama kuzikwa kama ingekuwa hivyo..
Baridi lililovuma kutoka usawa wa ziwa Victoria lilichangia zaidi Betty kutetemeka huku meno yakigongana kinywani, nguo yake nyepesi iliruhusu kila aina ya karaha, wakiwemo mbu. Kanga yake alikuwa amefunikwa mama yake mzazi ambaye alikuwa akiishi kwa chembechembe masalia za damu katika mwili wake. Maskini mama yule kabla ya kuwa kimya hakupata hata nafasi ya kusema neno la mwisho kwa mwanae. Labda neno moja lingejenga tumaini kuu la siku nyingi. Neno kutoka kwa mama mzazi.
Umasikini ulichelewesha hata teknolojia kupenya katika kijiji hiki, simu zilikuwa anasa. Alimiliki daktari na matajiri kadhaa kutoka mkoa wa Mwanza waliojihusisha na uvuvi wa samaki. Hii ilisababisha hata jamaa wa karibu wa familia ya Betty wasiweze kupata taarifa.
“Binti……” ilisikika sauti kutokea gizani, tayari ilikuwa saa moja na dakika kadhaa usiku. Betty akageuka na kukutana na kivuli kirefu, alipotazama kwa makini alikuwa ni daktari. Akapiga hatua kumsogelea.
“Kuna mbu wakali sana hapa, unaweza kupatwa hata na Malaria….” Alisema kisha akamsogelea zaidi na kuendelea .. “…nadhani ukajiunge na watoto wangu wa kike ujibane hivyo hivyo walau asubuhi tupate jibu kuhusu mama.” Sauti tulivu ya daktari ilimsemesha Betty. Badala ya kujibu, Betty akaanza kusina kisha kwikwi. Maskini Betty alikuwa analia.
Daktari akamsogelea na kukikumbatia kiganja chake cha baridi kilichopoteza uvuguvugu wa kike. Haikuwa mara ya kwanza daktari huyu kukipakata kiganja hiki. Mara ya kwanza alikuwa akimpa pole Betty baada ya baba yake kupoteza maisha katika vitanda vibovu vya zahanati hiyo pekee katika kisiwa cha Ukala.
Kule kuguswa na daktari kisha kupigwa pigwa begani, Betty akaikumbuka taarifa ya kifo cha baba yake. Kwikwi zikazidi, kadri alivyokuwa anazibana na kujaribu kupambana nazo mabega na kichwa chake vilikuwa vinapanda juu na kushuka huku akitetemeka.
“Pole sana binti…” daktari akatamka na hapo akawa amekifungulia kilio kikubwa kutoka kwa Betty. Daktari alitaka kumtuliza lakini akasita ili asije akamliza zaidi. Badala yake akamsogelea na kumnong’oneza.
“Mama atapona usihofu..” neno hili kwa kiasi fulani likamrudisha Betty katika hali ya kawaida. Daktari akamkokota hadi nyumbani kwake, nyumba isiyokuwa na umeme lakini walau taa za kandili zilileta Nuru.
“Mama Kezirahabi…..” aliiita daltari, sauti ya mwanamke kutoka jikoni ikaitikia kwa heshima kabisa. “Kuna mgeni wako huku..” alimalizia daktari na tayari mama kutoka jikoni alikuwa amefika.
Daktari Kezirahabi akamweleza mkewe juu ya uwepo wa Betty kwa usiku ule, mama mkarimu akampokea kama mwanaye wa kumzaa, akampatia chakula kilichokuwa kimesalia. Betty akajilazimisha kula, mama yule akamtia moyo sana. Majira ya saa tatu akamwongoza katika chumba cha wasichana aweze kupumzika.
Wawili hawa walipokelewa na mikikimikiki ya Panya waliokuwa wameutawala ukumbi baada ya wahusika kuwa wamesinzia. Jambo hilo halikumshtua Betty. Ile ilikuwa hali halisi ya maisha katika kijiji chao.
“Lala na wenzako mwanangu….we Jeni, Jenii….” Mama alimtikisa msichana mmoja akainuka na kisha kumpa maelekezo.
Wakajibanabana Betty akalala huku akikiri kuwa mama yule hakika alikuwa na upendo wa dhati. Upendo wa mama.
Baada ya kandili kutoweka, vita dhidi ya mbu wakali ikafuata. Japo palikuwa nyumbani kwa daktari hali ya kimazingira ilikuwa utata. Cha kushangaza hao mbu alijikuta akipambana nao peke yake, wenzake watatu walikuwa wanakoroma.

Jane ndiye aliyegundua utofauti asubuhi katika mwili wa mgeni waliyelala naye. Wadogo zake wawili hawakujua lolote juu ya afya ya mwanadamu. Alipomaliza kuwaandaa ili waende shule hakuweza tena kumezea suala la yule mgeni. Alikuwa anatetemeka sana wakati hapakuwa na baridi kali la kutisha. Jane mtoto wa kwanza wa daktari Kezirahabi akaifikisha taarifa kwa mama yake mzazi. Mama yule mwenye upendo akawahi upesi kule chumbani. Mama mkongwe aliyeolewa na daktari hakuhitaji vipimo kutambua kuwa binti yule yu katika mahangaiko mwilini akiibeba Malaria. Aliwaza hili, sit u kwa kuwa amewahi kuwashuhudia wagonjwa wa Malaria, bali kwa sababu usiku ule binti mgeni hakujipakaa mafuta yenye dawa ya kupambana na mbu waenezao malaria.
Upesi Betty akanyanyuliwa, mama akautega mgongo wake Betty akapanda akazungusha mikono yake na kumkumbatia. Upesi akamkimbiza katika zahanati ya mume wake.
Betty aliona kila kitu kilichokuwa kinaendelea lakini hakuweza kusema lolote. Kwa macho yake walipokaribia zahanati aliiona baiskeli ya kaka yake Jane. Aliitambua kutokana na bango lililokuwa likining’inia kwa nyuma. “MASIKINI HAPENDWI”…..Joyce akajaribu kutabasamu lakini hakuweza.
Akaingizwa katika wodi, humo akakutwa mgonjwa mwingine akiwa amelazwa na ndugu zake wamekizunguka kitanda. Wodi pekee iliyokuwa wazi ni ya wanaume, mama akafanya maamuzi akamuhifadhi upesi kitandani na kukimbilia chumba cha daktari kwenda kumpa taarifa.
Daktari alikuwa ametingwa na jambo lililohitaji uangalifu mkubwa. Bila kuvaa mavazi yoyote ya kazi yule muuguzi mstaafu akatwaa dawa na maji akakimbilia katika chumba alichokuwa amemlaza Betty. Betty akameza zile dawa bila kuchukuliwa vipimo.
Dawa maalum kwa ajili ya kutibu Malaria ambazo ni daktari na mkewe walitambua mahali zinahifadhiwa.
Baada ya masaa kadhaa hali ya Betty ikapata ahueni kiasi. Kisha kuweza kusimama kabisa baada ya kuambiwa kuwa mama yake mzazi alikuwa anamuita. Akakurupuka kutoka katika chumba kile akiwa na kiherehere cha kutaka kujua kama anaota ama ni kweli mama aliyedhaniwa kuwa atakufa amemuita.
Hakika haikuwa ndoto lakini ulikuwa zaidi ya muujiza. Alitegemea kukutana na uso wa mama yake pekee lakini sasa haikuwa hivyo tena, alikutana na nyuso mbili zilikuwa zinatangaza uchovu waziwazi lakini bado zilitabasamu, lile tabasamu kutoka moyoni.
“Betty!!!”
“Joy!!!”
Walisogeleana kwa kutoamini kisha wakakumbatiana….mama Betty naye akaungana nao katika kumbatizi hilo.
Joyce alikuwa amempunguzia damu mama yake Betty kwa kulazimisha akipingana na fikra za mama na baba yake.
Mama Betty alikuwa hai tena…..jeraha likiwa limefungwa kitaalamu na yeye akiwa wima tena. Alikuwa anaongea kama awali.
Miguu ya Joyce ilikuwa imevimba sana, alikuwa amenyonga baiskeli kwa kilometa nyingi sana hadi kuifikia zahanati. Mikono nayo ilikuwa imeumuka…..lakini haya yote hakujali, alichojali ni uhai. Uhai wa mama Joyce. Na hakika alikuwa amefanikiwa kumuokoa.
“Joyce mwanangu….Mungu akubariki mwanangu….Joyce umeniokoa mimi nilikuwa nimekufa Joy..Joy ulikuwa umeishika roho yangu….umeiponya roho hii…Mungu akubariki sina jingine la kusema mama!!” mama Betty alianza kusema. Maneno yake yakaamsha kilio upya. Mama Kezirahabi naye alianza kulia kwa sauti. Lakini kilikuwa kilio cha furaha japo furaha ambayo haikukamilika bado.

Mshawasha wa kuonana na mama yake akiwa hai ulikuwa umemsahaulisha kabisa juu ya ile Malaria mwilini mwake, lakini baada ya damu kupoa na akili kurejea sawasawa kile kizunguzungu kikarejea upya tena, kichefuchefu na kichwa kikaanza kugonga.
Malaria hii ya sasa ilicharuka na kumpelekesha haswaa.
Mama Betty akaazima simu kwa daktari akapiga simu kwa ndugu zake mkoani Mwanza. Akamueleza juu ya hali ile ya hatari. Walau huyu ndugu alikuwa na uwezo kifedha.
Hatua za upesi zikachukuliwa.
Siku iliyofuata Betty akasafirishwa kuelekea Mwanza akiongozana na mama yake mzazi ambaye bado alikuwa na jeraha bichi mguuni.
Walitamani sana kumuaga Joyce lakini haikuwezekana kwa sababu mzee Kisanga alikuwa amemfungia ndani baada ya kumshushia kipigo cha uhakika kwa kosa aliloliita utovu wa nidhamu. Mama Joyce alipojaribu kumtetea naye alibamizwa kofi moja tu lililompopeza uelekeo kabisa na kukomesha kiherehere chake.
Joyce alikuwa matatani kwa kujaribu kuokoa maisha ya mama wa rafiki yake mpenzi…..
Urafiki uliotukuka!!!

Juma moja baadaye Betty mwenye afya kamili alirejea kijijini lakini si kwa lengo la kuendelea na maisha yale magumu. Mjomba wake kutoka Mwanza alikuwa ameamua kumchukua na kuishi naye.
Marafiki wawili wakakumbatiana, wakalia kama kwamba kuna msiba wa mzazi mmoja wao. Ilikuwa ngumu kuamini kuwa wanatenganishwa wakati urafiki wao ukiwa umefikia pomoni. Hali hii ilimsikitisha hata mzee Kisanga, baba mzazi wa Joyce lakini aliendelea kuikunja sura yake kama kwamba hakuna lolote linalotokea pale.
Hatimaye Betty akatoweka kama anayerejea baada ya masaa kadhaa lakini ikakatika miaka bila wawili hawa kuonana, hadi Joyce akakiri kuwa wasingeweza kuonana tena, hasahasa baada ya mama yake Betty naye kutoweka kijijini kuelekea mjini Bukoba kuwasabahi ndugu zake kisha akaipanda meli ya Mv Bukoba aende Mwanza kumsalimia Joyce.
Ile ajali mbaya isiyosahaulika nchini Tanzania, ajali ya meli ya MV Bukoba: na yeye ilimkumba akiwa ndani.
Mwili wake haukuweza kupatikana, labda uliliwa na samaki ma vinginevyo…..
Kizazi cha Betty kikatoweka rasmi Ukala. Katika namna ya kufadhaisha na kuumiza mioyo.

**BETTY ametoweka kisiwa cha Ukala, ametengana na rafiki yake mpenzi JOYCE……anasikitika kumwacha Joyce katika kisiwa kile lakini atafanya nini??? Hana namna anatoweka…..
**Mama Betty naye anamezwa na ziwa Victoria…….safari ya Joy kumwona Betty tena inaingia doa….yule ndugu yake wa pekee naye ametoweka.

***WATAKUTANA tena maishani?? Watakutana vipi??
***ROHO MKONONI??? Kwa nini Roho mkononi??
ROHO MKONONI 02 MTUNZI: George Iron Mosenya SEHEMU YA PILI "Kama shilingi 5000... Read more »walumitz.blogspot.com