0
  Hatimaye Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015), Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015) na Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015

.Baadhi wa wabunge waliochangia, waliitaka serikali kuanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha wazawa kushiriki shughuli za uchimbaji wa gesi pamoja na rasilimali nyingine zilizopo hapa nchini ili taifa liweze kunufaika nazo na kwamba mtaji usiwe kikwazo.
 Akitolea ufafanuzi suala la miswada hiyo kupelekwa bungeni kwa hati ya dharura, waziri wa katiba na sheria Mh Asharoze Migiro amesema mchakato wa miswada hiyo ulinza siku nyingi na wadau wote walishirikishwa na wapo baadhi ya viongozi wa halmashauri walipelekwa nje ya nchi kujifunza hivyo kazi ya bunge ilikuwa ni kuipitia na kama kuna maboresho iboreshwe kabla ya kusainiwa kuwa sheria.
  Waziri wa Nishati na Madini Mh Simba Chawene akihitimisha mjadala huo amesema lengo la miswada hiyo ni kuhakikisha inajenga mfumo imara wa kisheria kusimamia sekta ya mafuta na gesi ili mwekezaji aweze kupata stahiki yake nataifa liweze kunufaika huku akiwataka watanzania kuepuka ushabiki wa kisiasa katika mambo ya msingi
Leo hii imepitishwa miswada miwili, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015 na uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali za Madini Wakati Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015) ulipitishwa jana Jumapili.
  Miswada yote hii imepitishwa bila uwepo wa Kambi ya upinzani bungeni, baada ya kutolewa nje na wengine kutoka wenyewe kwa kile wanachodi kwamba Miswada yote hii imevunjwa utaratibu na kanuni za bunge katika uwasilishaji. 
  Hata hivyo idadi ya wabunge wanaohudhuria vikao hivyo vya bunge ikiwemo ya waliopitisha mswada huo imeendelea kupungua kwa kile kinachodaiwa kuwa wengi wao wako majimboni kutokana na presha ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu.

Post a Comment Blogger

 
Top