0
Viongozi wa UKAWA, kutoka kushoto ni Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba na James MbatiaWATANZANIA hususani wapenda mageuzi wametakiwa kutulia wakati vyama vya upinzani ambavyo vinaunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA), vikifanya mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya umoja huo.… (endelea).
Rai hiyo ilitolewa na mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi, (Chadema), alipokuwa akizungumza na mwanahalisi Online juu ya mchakato ambao unaendelea kwa UKAWA kwa lengo la kumpata mgombea urais.
Mbunge huyo msomi amesema  kwa sasa watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kusikiliza Ukawa wanamtangaza nani ili aweze kupeperusha bendera ya kuwania nafasi ya urais.
Mbali na hilo amesema  kuchelewa kwa upatikanaji wa jina la mgombea urais kupitia ukawa kumekuwa kukitumiwa na watu ambao hawana nia njema na umoja huo kwa kutoa maelezo kuwa ukawa wamesambaratika.
Amesema  Ukawa ni umoja unaoendeshwa na watu makini hivyo ni lazima kufanya mazungumzo ya kina zaidi ili kuhakikisha inapata  mgombea ambaye anauzika na anakuibalika ndani ya umoja huo na nje ya umoja huo kwa maana nay a wananchi.
Akizungumzia suala la Dk. John Magufuli kuwa mgombea urais kupitia CCM amesema  kwa sasa hakuna haja ya kuangalia mtu bali jambo pekee la kuangalia ni mfumo.
Amesema  serikali haiendeshwi na mtu mmoja hivyo Dk.Magufuli hawezi kuwa ndiye jibu la kutatua matatizo ya wananchi mfumo kama ni mbovu hata kama angekuja kiongozi mzuri namna gani hawezi kubadilisha jambo lolote.
“Nikweli Dk.Magofuli  ni mchapa kazi hata kama anayo mapungufu kama ilivyo kwa binadamu wengine, lakini kinachosumbua serikali ya CCM ni mfumo uliopo.
“Ufisadi wote unafanyika ndani ya serikali ya CCM na ili kuondokana na ufisadi na pamoja na ubadhilifu wa mali ya Umma ni lazimakufumua mfumo mzina .
“Sasa tujiulize ni wapi ambapo anaweza kufumua mfumo huo, rais wa Sasa Jakaya Kikwete alijaribu kutaka kuwavua wana CCM wenzao magamba lakini nini kilichofanyika na badala yake magamba hayo hadi sasa anamaliza muda wake bila kuyavua,” amesema  Prof. Kahigi.
Kutokana na hali hiyo Profesa Kahigi aliwataka watanzania kutokubali kudanganywa kwa siasa nyepesi kwa kuhaminishwa kuwa mtu mmoja ndani ya serikali anaweza kutatua matatizo ya wizi kama mfumo mzima haujabadilishwa.
Akisisitiza uchaguzi amesema  ili kuweza kupata viongozi waliobora ni lazima kufanya mageuzi ili mfumo mpya na safi uchukuemadaraka .
Amesema  kwa sasa ni lazima kiongozi wa CCM atumie mikataba mibovu ambayo imetengenezwa na serikali hiyo inayolenga kuwalinda wakubwa na kuwapatia fedha nyingi.
Amesema  mfumo wa sasa unasababisha kuwepo kwa kundi la wasiokuwa nacho kuongezeka huku kundi la wenye nacho wakineemeka na kundi hilo ni la watu wachache mno.

Post a Comment Blogger

 
Top