Kocha mkuu wa Manchester United  Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mshambuliaji mwingine kwani alio  nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.
Pamoja na  Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes  Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin  Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel  Falcao mkopo wake kumalizika.Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.
 
Post a Comment Blogger Facebook