0
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahilihood Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amekuwa kivutio kikubwa kati ya wagombea waliotangaza nia kugombea Jimbo la Kinondoni, msanii mahiri katika uchekeshaji na uigizaji wa sauti mbalimbali za watu maarufu Ulimwenguni ametangaza nia kugombea Jimbo hilo.
Steve akiwa na baadhi ya wasanii wenzake kutoka Bongo Movie waliingia ofisi za CCM Mkwajuni Wilaya ya Kinondoni na kupokelewa na kundi la wanahabari tofauti na wagombea wengine walioingia katika ofisi hizo na kumwaga sera zake huku kila mwanahabari akiwa na hamu ya kutaka kuongea naye kwani ameamua kujitosa katika Jimbo maarufu Dar.
“Ni wakati wa Vijana kuwakilisha jamii kwa kuingi kama watunga sera wakishiriki moja kwa moja katika kutetea na kuwatumikia wananchi hususani Jimbo la Kinondoni,”
“Kinondoni tumepata bahati ya kuwa na Balozi zote kubwa ni Wilaya yenye wakazi wengi kuliko hata baadhi ya Mikoa ukiongelea Burudani zote ni Kinondoni, sasa umefikia wakati wa kuifanya Kinondoni iendane na hadhi yake, na mtu pekee anayeweza kufanya hivyo ni Steven Wayton Mengele,”anasema Steve Nyerere.
Hadi sasa Steve Nyerere ndio mpinzani pekee anayetishia kunyang’anya nafasi kwa Mbunge aliyopo Idd Azan tofutti na wagombea wengine kwani imeonekana kuwa msanii huyu anaijua vema kisiasa Jimbo la Kinondoni na mwenye mvuto kuliko wagombea wote kwa Jimbo la Kinondoni.
Steve Nyerere kaonyesha uchapa kazi baada ya siku ya Ijumaa kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa ridhaa ya Chama cha Mapinduzi na kuijaza siku hiyo hiyo na kuirudisha na kuonyesha kuwa na nia yadhati katika suala hilo muhimu katika mustakabali wa Taifa.

Post a Comment Blogger

 
Top