0

BAADA ya kikao (summit) kukamilisha maridhiano ambapo kilizungumzia jinsi gani ya kuachina majimbo yalibaki na suala la mgombea urais, sasa mgombea urais ndani ya UKAWA kuja kutangazwa kwa shamrashamra ndani ya siku saba.
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia aliwaeleza wanahabari kuwa taratibu zote zimekamilika ndani ya vyama vinavyounda UKAWA na kilichobaki ni jinsi gani ya kumtangaza mgombea urais ndani ya UKAWA kwa kushirikiana na vyama vyote vinavyounda umoja huo, ndani ya siku saba.
Huku akiwasisitiza Watanzania kuwa wavumilivu na kuwataka wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotegemewa kuanza hivi karibuni katika Mkoa wa Dar es Salaam huku wakitega masikio yao na kumpokea mgombea urais ambaye atatambulishwa kuipeperusha bendera kupitia UKAWA.
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyeuliza kuwa, Je, ni kweli kama ilivyotapakaa katika mitandao ya jamii juu ya Lowassa kujiunga na chama kimojawapo ndani ya vyama vinavyounga UKAWA?
Akijibu swali hilo kwa kulitolea mifano ya mitandao ya jamii inayotumika na watu fulani kwa maslahi yao binafsi na siyo kuelimisha jamii, Mhe. Mbatia alizungumzia moja ya akaunti ya Twitter iliyofunguliwa kwa jina la mtandao mkubwa duniani BBC ikieleza kuwa Lowassa tayari ameshajiunga katika Chama cha ACT na kusisitiza habari hizo siyo za kweli huku akiwashauri Watanzania kupima uzito wa habari na chombo kinachoiwasilisha na kuwataka wananchi wafuatilie habari za vyama kupitia mitandao ya vyama hivyo.

Post a Comment Blogger

 
Top