0
Prof. Mwandosya ambaye alikuwa mmoja wa wagombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye jina lake liliondolewa katika hatua za awali za kinyang’anyiro hicho anasema, “ni muhimu kama viongozi, kuvumiliana na kuheshimiana,” ili taifa lisiingie katika machufuko.
Akiandika katika ukurasa wake wa facebook, Prof. Mwandosya amesema, taifa linapita katika kipindi kigumu, hivyo ni vema wanasiasa na wananchi wengine wakajenga utamaduni wa kuvumiliana.
Amesema, “katika kipindi hiki muhimu, kama taifa, inatupasa tuzingatie; kuvumiliana, kuheshimiana, kukubaliana, kukubali kutokubaliana, kushindana kwa hoja, na kutumia lugha yenye staha.”
Prof. Mwandosya anasema, “Msaafu Mtakatifu unatukumbusha ‘…vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao huvuna majivuno makuu.”
Andishi la Prof. Mwandosya limekuja siku tatu baada ya Mkapa kufungulia bomba la matusi kwa kuwaita viongozi wakuu wa upinzani nchini na wafuasi wao, kuwa marofa na wapumbavu.
Mkapa alisema wapinzani wanaosema vyao vyao ni vya ukombozi ni wapumbavu na malofa kwa kuwa Tanzania ilishakombolewa na vyama vya Tanganyika National Union (Tanu) na Afro Shirazi Party (ASP).
Bila kutaja jina la Mkapa, Prof. Mwandosya aandika kwa njia ya kuonya, “…angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana…”
Anasema, “Msaafu Mtakatifu unatuonya pia “…kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa….”
Tangu Edward Lowassa, kujiunga na upinzani na baadaye Fredrick Sumaye, kumfuata kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuondoa CCM madarakani, kumekuwa na mihamko ya viongozi wakuu wa chama hicho na serikali kuzuia upinzani kushika dola.
Taarifa zinasema, mihamko hiyo, ndiyo iliyomsukuma Mkapa kutukana baada ya kuona kitumbua chake kinaingia mchanga.

Post a Comment Blogger

 
Top