0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeazimia kutoa vitambulisho vipya vya taifa vyenye saini kwa wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili.
tanzania_refugee_
Taratibu hizo ni pamoja na kuchukuliwa alama za kibaolojia, ikiwemo alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Andrew Massawe, ametoa taarifa hiyo na kusema kwa sasa vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya huku taratibu za kuvibadilisha zikiendelea.
“Kutokana na uwepo wa njia nyingi na salama za kusoma taarifa za mwombaji zilizomo ndani ya kifaa maalumu kilichofichwa kwenye kadi ya mtumiaji, ndiyo maana vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika katika huduma mbalimbali zinazohitaji kumtambua mtumiaji kabla ya kupata huduma,” alisema Massawe.
“Kwa wale ambao walisajiliwa kupitia daftari la kudumu la mpiga kura la tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), NIDA iko mbioni kuanza kutoa nambari za utambulisho wakati taratibu za uzalishaji zikiendelea,” aliongeza.
Kwa wananchi ambao tayari wana vitambulisho visivyo na saini, Massawe amesema,” mamlaka inakusudia kubadilisha vitambulisho vyote vya zamani visivyo na saini, ila kwa sasa vitambulisho vya zamani vitaendelea kutumika sambamba na vipya wakati taratibu za kuendelea kuvibadilisha zikiendelea,” alisisitiza.
Aidha Massawe alisema kuwa ofisi za wilaya zilizoanza usajili wa vitambulisho hivyo vipya kwa Tanzania Bara na Zanzibar ni mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma na Dodoma.
Mamlaka hiyo inatarajia kutoa vitambulisho vipya kuanzia Septemba 14, mwaka huu katika ofisi zote za NIDA za wilaya.

Post a Comment Blogger

 
Top