0
Klabu ya Chelsea Alhamisi hii imetangaza rasmi kuwa wameingia mkataba na kampuni ya utengenezaji vifaa na jezi ya Nike,utakaoanza msimu wa 2017/2018.
chelsea
Imeripotiwa kuwa mkataba huo ni wa miaka 15 na una thamani ya pauni milioni 60 kwa mwaka, wakati mkataba wao wa sasa wa Adidas una thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka.
Chelsea wamekuwa na mkataba na Adidas tangu mwaka 2006 na hivyo imewalazimu kuilipa kampuni hiyo pauni milioni 40 ili kuvunja mkataba wao ambao unamalizika mwaka 2023.
Mkataba huu unaifanya Chelsea kushika namba 2 katika timu zinashoriki EPL, namba 1 ikiwa ni Manchester United ambao mkataba wao na Adidas una thamani ya pauni milioni 75 kwa mwaka, huku Arsenal wakishika namba 3, mkataba wao na puma una thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka.

Post a Comment Blogger

 
Top