0
Mwanzilishi mwenza wa label ya Roc-A-Fella Records, Kareem ‘Biggs’ Burke amezungumzia dongo la Kanye West kwa swahiba wake, Jay Z.
398eea8900000578-3865720-shade_he_said_jay_z_did_not_visit_him_after_his_wife_kim_kardash-a-51_1477279632188
“Nilishtuka kusikia kile Kanye alikisema jukwaani,” alisema Burke wakati wa kuadhimisha miaka 20 ya album ya Jay Z, Reasonable Doubt.
West alimchana Jay Z kwa kushindwa kwenda kumsalimia baada ya mke wake Kim Kardashian kuvamiwa Paris na kudai kuwa watoto wao hata hawajawahi kucheza pamoja.
Burke aliimbia Page Six: “Mara ya mwisho nimemuona [West], aliongea mazuri kuhusu Jay. Sina uhakika na uhusiano wao ulivyo sasa. Niliongea na Jay baada ya Kanye kusema vile na wote tulisema ‘tunammiss Kanye wa zamani.”
“Kwa jinsi ninavyomjua Kanye, siku zote huwa msema kweli. Kwahiyo inaonekana kuna kitu kinamsumbua sasa hivi. Anaweza kusema kitu kama hicho na kisha wiki tatu baadaye anaweza kurudi na kusema, ‘That’s my brother.’ Lakini katika hatua hii tuliyofikia, tumekuwa wakubwa mno kuwa na bifu za rap.”

Post a Comment Blogger

 
Top