0
Mchezaji ghali zaidi kwasasa duniani kiungo Paul Pogba amesema kuwa anapenda kocha Jose Mourinho amchezeshe mbele zaidi katika kikosi cha Man United.
57d5732685d7c_pogba
Tangu aliporejee katika klabu ya Manchester United kwa pauni milioni 89, Pogba amekuwa akichezeshwa chini zaidi katika sehemu ya kiungo, akifanya majukumu ya ulinzi.
Amesema kuwa kuchezeshwa chini zaidi katika sehemu ya kiungo katika klabu ya Man United, kuna mgharimu sana.
Katika mechi ya Ufaransa dhidi ya Uholanzi baada ya kucheza juu zaidi kwenye sehemu ya kiungo katika mechi ya jumatatu hii iliyopita, kiungo huyo alionesha uwezo mkubwa na kufunga goli zuri ambalo liliipa timu yake pointi 3.
“Ninajitahidi kuzoea,” Paul alisema hayo wakati akiongea na Manchester Evening News.
“Mimi ni mchezaji ninayependa kwenda mbele. Kocha ananipa maelekezo najaribu kuyafuata. Inabidi nirudishe mipira na kufanya majukumu ya ulinzi.
‘Inanigharimu sana kucheza tofauti, kama vile achezavyo Andrea Pirlo.’

Post a Comment Blogger

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top