0
UONGOZI wa Azam FC umemtengea dola elfu 70,000 kwa mshambuliaji wa Gor Mahia Michael Olunga na mshahara wa dola elfu nane ili aweze kutua katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo ambaye anawaniwa na pia na Simba ameonekana mshambuliaji hatari katika michuano hiyo, baada ya kuonyesha uwezo kwa kufunga mabao matatu katika michezo miwili.
Simba awali walitangaza kumsajili mchezaji huyo kwa dola 20,000.
Habari kutoka ndani ya Azam FC zilieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umetenga dola hizo, baada ya kuambiwa kuwa uongozi wa Gor Mahia umewataka Simba kutoa dola elfu 50,000 ili waweze kumpata mchezaji huyo.
Mtoa habari huyo alisema azam FC wameanza mazungumzo na Gor Mahia kama wanaweza kukubali kumuachia mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo.
Alisema kama Azam FC watampata mchezaji huyo wataradhimika kukatisha mkataba na mshambuliaji wao kutoka Burundi Didier Kavumbagu ambaye kiwango chake kina suasua kwa kuwa wamefikisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
Azam FC ina wachezaji wa kigeni saba ambao ni Kavumbagu (Burundi), Pascal Wawa, Kipre Tchetche, Kipre Bolou (Ivory Coast) Allan Wanga ( Kenya) Jean Baptiste Mugiraneza (Rwanda) na Brian Majwega.
Ofisa Habari wa Azam FC Jaffar Idd alisema kuwa klabu yao kwa sasa haina mpango wa kusajili mchezaji yoyote kutoka nje ya nchi kwa kuwa wamefikisha idadi ya wachezaji saba ambao wanatakiwa.
Azam FC ambao wanaongoza kundi C wakiwa na pointi sita kesho itashuka dimbani dhidi ya Adama City ya Ethiopia.

Post a Comment Blogger

 
Top