0
Viongozi wa UKAWA
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimekanusha uvumi  kuwa   kimejiengua na kukisusia kikao kinachoendelea cha Umoja wa Katiba ya Wananchi  (UKAWA),  kwa kile kinachodaiwa  kina uchu  wa madaraka. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Aidha, CUF imekanusha uvumi  kuwa baadhi ya wananchama na wenyeviti wa CUF kununuliwa na Chama cha Mapinduzi ( CCM), kwa lengo la kuuvuruga umoja wao na kuisambalatisha UKAWA.
Hayo yamebainishwa  leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari ambamo kimechukua fursa hiyo kuwaonya   waandishi kuandika habari za kweli  zinazohusu UKAWA kuliko kuandika habari zinazoweza kupotosha umma.
Sakaya ameendelea kusisitiza kuwa, CUF haijajiengua na UKAWA, ambamo amebainisha sababu za kutoshiriki katika kikao cha jana Julai 14,2015 kilichofanyika katika ukumbi wa Collesium Dar,  kumetokana na sababu za kikatiba za ndani ya Chama ambapo jana walikaa kikao hivyo kupelekea kushindwa kutuma mwakilishi katika kikao hicho.
“Baada ya kikao cha UKAWA cha Julai 11 mwaka huu CUF tumekuwa  na vikao vinavyohusu viongozi wakuu wa Chama akiwemo Mwenye kiti, manaibu katibu wakuu na wakurugenzi na jana ndo tulikuwa na kikao na ndio maana hatukuweza kutoka” amesema Sakaya.
“Kutohudhura katika kikao cha jana hakuna mahusiano yoyote na uvumi na maneno ya chini chini kwa baadhi ya mitandao ya kijamii yanayopotosha umma”
Kuhusu uvumi unaodai kuwa UKAWA umeshampitisha mgombea kwa kupiga kura na kwamba baadhi ya magazeti kumuandika mgombea amesema halina ukweli, taarifa hizo pia zilipelekea  baadhi ya wananchama  wa CUF kukusanyika makao makuu ya CUF ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya uvumi huo.
 Nae Mkurugenzi mipango na uchaguzi Shaweji Mketo amesema, kuhusu  maneno yanadai kuwa UKAWA ni pasua kichwa  na kwamba unakaribia kuvunjika hayana ukweli  isipokuwa wanafuata katiba ya kila chama ndipo wamtoe mwali atakaye peperusha bendele ya UKAWA.
Amesema, “niwatoe wasiwasi wananchi na wapenzi wa UKAWA muondoe hofu tupo imara na tunatarajia baada ya siku tano kumtangaza mgombea wetu, na kikubwa kinachojadiliwa sasa ni ugawaji wa majimbo kutokana na kuongezeka kwa majimbo hivyo ni lazma tuyajadili kwa kina na kujua yupi atachukuwa wapi”
Kuhusu kikao cha Baraza  kuu la uongozi wa kitaifa  Mketo amesema, “tunatarajia kufanya kikao cha mwisho Julai 25 mwaka huu ili kupata Baraka  ya chombo cha maamuzi kama ambavyo wezetu wa washiriki wa UKAWA wamekwisha pitia hatua hizo katika vyama vyao”

Post a Comment Blogger

 
Top