0

Mwigizaji wa filamu za vichekesho wa Kenya Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang (pichani) amefariki dunia Jumapili jioni katika hospitali ya Taifa ya  Kenyatta National alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Taarifa kutoka NAirobi zinasema alikuwa anaumwa "Nimonia" (Pneumonia). 

Marehemu Mzee Ojwang alijipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa vituko vyake kwenye filamu za Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na  Kinyonga. Alikuwa haonekani kwa muda mrefu kwenye televisheni za Kenya na mashabiki wake wakiwemo wa Tanzania walikuwa hawaishi kumuulizia aliko bila kupata jibu. 

Mola aiweke Mahali pema roho 

ya Mzee Ojwang - Amin.

Post a Comment Blogger

 
Top