0
Diamond ni msanii mkubwa kwa sasa, lakini naye amepitia mwanzo mgumu kabla ya kuanza kuyaona mafanikio aliyonayo.

Kwa kutambua ugumu wanaokutana nao wasanii chipukizi, rais huyo wa Wasafi ameamua kuwasaidia wasanii wachanga kwa kuwapa nafasi ya kurekodi bure katika studio yake mpya aliyofungua ‘Wasafi Records’.

“Lengo maalum la kufungua studio ‘Wasafi Records’ sio nimelenga biashara itakuwa uongo” alisema Diamond kupitia kipindi cha The Jump Off kupitia Times Fm. “…Lakini hiyo studio nilivyokuwa nimeiweka nimesema arekodiwe msanii yeyote mwenye kipaji, akiwa mtu ana kipaji kizuri ana nyimbo nzuri mrekodie mpe. Lakini pia iko na kibiashara kwa wasanii wengine sio msanii ameshatoka aje pale aimbe bure, hamna wakishatoka hela wanazo waje walipe hela.”

Diamond ameongeza kuwa pia atakuwa anasimamia wasanii ambao atawachagua mwenyewe kulingana na kipaji cha msanii, na tayari kuna msanii yuko chini ya label yake.

“kuna wasanii ambao watakuwa chini ya management yangu chini ya kampuni yangu mfano huyu anaitwa Hamonizer.”

Msanii mwingine wa Tanzania ambaye alisema ana mpango wa kusaidia wasanii wachanga kwa kuwasimamia ni pamoja na Ommy Dimpoz, kupitia kampuni yake ya ‘PKP’ Poz Kwa Poz.

Post a Comment Blogger

 
Top