0
Rapper Inspector Haroun amesema kuwa ameamua kuboresha kazi zake mpya za muziki kwa kurekodi nyimbo tatu mpya na watayarishaji wa muziki kutoka Afrika Kusini.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni akiwa Afrika Kusini, Inspector alisema ameamua kufanya hivyo ili kuleta ladha mpya kwenye muziki wake.

“Tayari nimeshaongea na producer wa South na sasa hivi najipanga kuingia studio kwa kuanza kurekodi. Muziki wa sasa hivi umejaa ushindani na unahitaji ubunifu wa aina fulani ndio maana unaona tunahangaika huku na kule ili kupata ladha tofauti,” alisema Inspekta.

Pia Inspekta alisema akishamaliza kurekodi kazi hizo ndio atajua anafanya video za aina gani huku akiwataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula.
Source BONGO

Post a Comment Blogger

 
Top