0
WANACHAMA wa kundi la Marafiki wa Edward Lowassa waliochanga fedha za kumwezesha waziri mkuu huyo wa zamani kuchukua fomu ya kugombea urais, wamemtuhumu aliyekuwa naibu katibu wao, George Kivuyo  kutafuna fedha hizo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wanachama hao wanaojulikana kama Team Lowassa 4 President, zinadai naibu katibu mkuu huyo ambaye pia ni mweka hazina wao, alitafuna kiasi cha shilingi laki saba zilizochangwa.
Walidai fedha hizo ziligunduliwa kutotumika ilivyopaswa baada ya kutojulikana zilipo na alipoulizwa hakuwa na majibu ya kueleweka.
Baadhi ya wanachama hao, Fauzia Ally, Hassan Mollel na Yussuf Hamis walisema kutokana na kitendo hicho, wanachama hao wameanza kufarakana kutokana na mgogoro.
“Hizi fedha zilitumiwa tofauti na ilivyokusudiwa, zinatakiwa zirudishwe, akabidhiwe mzee Lowassa,” alisema Hassan Mollel.
Naibu katibu mkuu huyo alipopigiwa simu na mwandishi wetu juzi Jumapili alisema kwamba madai hayo ni ya uongo na fedha hizo hazikuwa laki saba bali zilikuwa Sh. 526,000.
“Mimi ni mweka hazina msaidizi na tatizo limekuja baada ya kuhoji kuhusu fedha hizo alizokabidhiwa bosi wangu.”
Katibu mkuu wa chama hicho, Mohamed Mkindi alipoulizwa alikiri kusikia malalamiko hayo lakini alidai yupo mikoani na akirudi jijini Dar es Salaam atazifuatilia.

Post a Comment Blogger

 
Top