0
Maoni ya baadhi ya wanachama wa CUF juu ya uraisi ukawa

Wadau ni muda mrefu tangu mheshimiwa Lipumba achaguliwe rasmi na chama chetu cha CUF kuwa mgombea urais.

Ukizingatia hasa weledi wako uzoefu wako na uvumilivu wako na staha katika siasa unafaa kabisa sasa kupokea kijiti hiki safari hii. Ni mzoefu katika uchumi, umewahi kuwa mshauri wa Rais mwinyi na Museveni wa uchumi na kabla ya hapo umefundisha wachumi wetu wengi ambao Taifa sasa linawategemea. Wewe ni msafi na si mfanya biashara . Yaani una tunu zote za uongozi. Tatizo moja tu dogo ulilonalo labda la udini kidooogo. Kwa hili nakuomba usiendekeze. Kaa nalo mbali ili uweze kuleta imani hata kwa wale wa upande mwingine.

Naomba nikushauri na uelewe kabisa kuwa wewe huwezi linganishwa na hawa wafanya biashara wakina Mbowe na Dr.Slaa. Kamwe you cannot sail in the same boat, never. Umewapita mbaali sana nashangaa eti katika ukawa wanataka kukutosa usiwe mgombea urais. Ni ajabu na kweli. Kwa kisingizio eti huna umaarufu na mvuto kwa watu.

Mbona Lowasa amekuwa na mvuto kwa watu na bado amekatwa. Achana nao kabisa hao wachumia tumbo ambao wanataka kupata uongozi kwa maslah binafsi na si kwa maslahi ya wengi. Tangu lini mfanya biashara akawa na lengo la kuendeleza watu badala ya kujinufaisha mwenyewe. Always a businessman will want want to maximize his incomw indefinete.

Nachokiona wanataka kukupoteza na chama chako makini kwa faida yao na nakutahadharisha endapo utaamua kujitosa nao soon or later chama chako ujue ndio kitaelekea shimoni. Kitafutika katika ramani ya Tanzania na mwishowe kitakuwa kama TLP au UDP au NLD.

Tafakari chukua hatua.

Naomba Prof email yako ili nikupe mtizamo chanya

Post a Comment Blogger

 
Top