0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Majohe, Gekura Gisiri, amejiuzulu baada ya mgombea wa udiwani kwenye kata hiyo, Hassan Kingalu aliyekuwa akilalamikiwa kutoa rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni kutangazwa mshindi atakayegombea udiwani wa kata hiyo.
Pamoja na hatua hiyo ya kujiuzulu, wananchi wa eneo hilo nao wameonyesha kutokukubaliana na kupitishwa kwa mgombea huyo, kwa kudai kuwa hana sifa za kuwa kiongozi wao.
Mwenyekiti huyo wa CCM kata ya Majohe, Gekura Gisiri aalipozungumza na Star Tv amedai kuwa pamoja na kuwasilisha malalamiko hayo wilayani, lakini hakupewa ushirikiano wa kutosha, hali iliyochangia kufikia hatua hii.


wananchi wa kata ya majohe waliokusanyika pamoja kwa ajili ya kupinga uteuzi huo nao wakazungumza na Star Tv.
 kutokana na hali hiyo mgombea udiwani kupitia chama cha mapinduzi kata ya Zingiziwa Abdilah Mpate amewataka wanaCCM kuwa kitu kimoja hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ili kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi na wala siyo kuleta mvurugano.
 Kumekuwepo na malalamiko ya hapa na pale, tangua kuanza hadi kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni, na kusababisha wanachama kuchukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwakataa hadharani washindi kwenye kinyang’anyiro hicho.

Post a Comment Blogger

 
Top